TANGAZO


Saturday, September 27, 2014

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara afungua warsha ya siku mbili ya masuala ya Maafa Mtwara

MKUU wa Wilaya ya Mtwara Bw. Wilman Ndile, akifungua warsha ya siku mbili ya masuala ya maafa, Mtwara.
Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Fanuel Kalugendo akieleza lengo Tathmini ya Viatarishi, Uwezekano wa Kuathirika na Uwezo wa Kukabiliana na Maafa yaani (Risk Vulnerability and Capacity Assessment - RVCA), wakati wa warsha ya siku mbili iliyofanyika Septemba 26 na 27, 2014  kwa wadau wa Maafa  wa Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika warsha hiyo.


MKUU wa Wilaya ya Mtwara Bw. Wilman Ndile ameifungua Warsha ya Siku Mbili Wilayani Mtwara kuhusu “Mpango wa Kujikinga, Kukabiliana na Kuzuia athari za Maafa kwa Wilaya ya Mtwara juzi tarehe 26 na 27 Septemba, 2014. 

Wakati wa ufunguzi huo Bw. Ndile alisema Mpango huu utasaidia sana pindi maafa yatakapotokea na kuwaomba washiriki wa warsha hiyo kutoka Manispaa na Halmashauri ya Wilaya hiyo kushiriki vema katika mafunzo na kuchangia masuala hayo ili kuweza kukamilisha mpango huo unaoratibiwa na Idara ya Uratibu wa Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu.

Alisema “hatua hizi zimekuwa madhubutu na zitatusaidia sana sisi kama wadau wakubwa wa Maafa katika Halamshauri zetu na Manispaa kwa kuona uzito wa  suala la Maafa ni la kila mmoja na sio Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye ni mratibu tu wa Maafa” alisisitiza Bw. Ndile. 

Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Waziri Mkuu

26 Septemba, 2014, Mtwara

No comments:

Post a Comment