TANGAZO


Thursday, September 18, 2014

Kinana atembelea Shule ya WAMA-NAKAYAMA Rufiji mkoani Pwani

*Ampongeza Mama Salma kwa kuanzisha shule hiyo iliyopata ufaulu mzuri kidato cha nne

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Adbulrahman Kinana akizungumza na wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA, aliposimama kwa muda akitokea ziara ya Kisiwa cha Mafia kwenda Dar es Salaam. Alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kitendo cha kuanzisha shule hiyo, yenye manufaa makubwa kwa watoto ya kike wanaotoka sehemu mbalimbali nchini kwenda kusoma hapo. Pia alitumia furssa hiyo kuwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanaoifanya kiasi cha kufanikisha wanafunzi kufanya vizuri katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana. (Picha zote na Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio Blog) 
Mkuu wa shule hiyo, Suma akielezea historia ya shule hiyo inayofundisha watoto wengi yatima.
Wanafunzi wakifurahia pongezi za ufaulu mzuri zilizotolewa na Kinana.
Moja ya majengo ya shule hiyo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaimbisha wanafunzi wa shule hiyo, wimbo wa 'Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote', uliotungwa enzi hizo na babake Moses Nnauye.
Wanafunzi wakishangilia kwa furaha baada ya kuimba bila matatizo wimbo huo.

No comments:

Post a Comment