Walimu wa Shule ya Sekondari ya Viwandani wakijaribu kumdhibiti mmoja wa vijana waliofika katika sherehe za mahafali ya kidato cha nne, aliyefika na wenzake na kisha kuanzisha fujo kwa kupiga watu hovyo kwa mawe hali iliyosababisha Mwalimu wa Shule hiyo, Mwanafunzi na Mwandishi wa habari wa kituo cha Rasi Fm aliyekuwa kwenye majukumu yake kujeruhiwa kichwani.
Baadhi ya wazazi, walezi na wageni mbalimbali waliofika kwenye mahafali hayo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea kwenye mahafali hayo juzi.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Simu ya Airtel, Anthony Msanga akitoa hutuba kwenye mahafali ya sita ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Viwandani, walioka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Zainab Rajab na Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Oliver Masangia.
Mhitimu wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Viwandani Annastazia Bukola akionyesha kipaji cha kuimba na kucheza Muziki wa Kizazi kipya huku wahitimu wenzake wakimshangilia, ambapo aliibuka na zawadi ya Mordem ya Airtel yenye kifurushi chake ili aweze kuingiza nyimbo zake kwenye mitanadao ya kijamii ili kipaji chake kiweze kujitangaza mapema.
Mgeni rasmi kwenye Mahafari ya 6 ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Viwandani, Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya Kati, Anthony Msanga akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu wakati wa mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Viwandani, Manisapaa ya Dodoma wakiwa katika mahafali hayo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Viwandani, Manispaa ya Dodoma, Zainab Rajab akisoma taarifa ya shule hiyo, kwenye mahafali ya 6 ya kidato cha nne, yalihusisha wahitimu 115. (Picha zote na John Banda, Dodoma)
No comments:
Post a Comment