HATUA mahususi na za haraka zinahitajika kukabiliana na ugonjwa wa saratani ambao umegeuka kuwa tishio hapa nchini.
Hayo yalisemwa na daktari bingwa wa
ugonjwa huo, hususani saratani ya matiti kutoka India, Profesa Anthony
Pais, jana jijini Dar es Salaam katika majumuisho ya ziara yake
aliyoifanya katika mikoa mbalimbali kuangalia ukubwa wa ugonjwa huo.
Akiwa ameongozana na viongozi wa kampuni ya Mabibo Beer Wines and
Spirits Limited, iliyodhamini ziara hiyo, daktari huyo ameshauri kuwa
kuna umuhimu wa kujenga kituo kikubwa cha kimataifa hapa nchini
kitakachoshughulikia ugonjwa huo ili kupunguza gharama za kupeleka
wagonjwa nje ya nchi.
"Nimegundua kuna vituo viliwili, kimoja
Ocean Road na Hospitali ya Muhimbili. Lakini tatizo la saratani kwa sasa
Tanzania ni kubwa na linahitaji kushughulikiwa kwa haraka. Ningependelea
kuwepo na vituo viwili vikubwa, kimoja Mwanza na kingine Bukoba, ili kuhudumia hata nchi jirani," alisema.
Ameeleza kuwa katika ziara aliyoifanya
katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Kagera na Mwanza, amegundua kuwa kuna
aina kuu tatu za saratani ambazo zinasumbua wananchi wengi na
kumekuwepo na msululu wa wagonjwa wakipelekwa India kupata matibabu kwa
gharama kubwa.
Dk. Pais amezitaja aina hizo za saratani
kama saratani ya matiti, saratani ya kibofu cha mkojo na saratani ya
shingo ya uzazi. Alieleza kuwa wagonjwa wengi wamekuwa wakigundulika
kuwa na saratani hizi wakati tayari zimeshafikia hatua ya kutisha.
"Hivyo tukiwa na vituo hapa hapa
Tanzania vya kupima na kutibu ugonjwa huu itasaidia wagonjwa kujulikana
mapema na baadae kupata tiba haraka tena kwa bei nafuu. Mimi niko tayari
kutoa mafunzo kwa wahusika mbalimbali kutoka madaktari hadi wahudumu.
Kwa pamoja tunaweza," alisema.
Naye Mshauri wa kujitegemea wa kimataifa
wa Mabibo, James Rugemalira, ambaye kampuni yake husambaza vinywaji
aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught hapa nchini, amemshukuru
daktari huyo kwa kukubali kuja na kwa ushauri wake ambao utasaidia sana
katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Ameeleza kuwa mara kampuni yake
itakapopokea taarifa ya kitaalaam kutoka kwa daktari huyo, Mabibio
itaaanzia mchakato utakaofanikisha ujenzi wa vituo vingine vya
kushughulikia ugomjwa wa saratani ili kupambana na tatizo hili hapa
nchini.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea,
James Rugemalira (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari wakati wa majumuisho ya ziara ya Profesa Pais ya kutembelea
mikoa kadhaa nchini. Kutoka kulia ni Dk. Sima Rugarabamu wa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and
Spirits LTD, Benedicta Rugemalira na Profesa Pais.
Profesa Pais (kushoto), akitoa majumuisho ya ziara yake hiyo. Kulia Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits LTD, Benedicta Rugemalira, ambayo ilidhamini ziara hiyo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kushoto) na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits LTD, Benedicta Rugemalira
(kulia), wakimpa zawadi Profesa Pais baada ya kutoa majumuisho hayo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Waandishi wa habari, ambao ni Mabloga, wakiwa katika hafla hiyo. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Blog hii ya bayana, Kassim Mbarouk, akiwa kazini.
Wadau wa sekta ya afya wakiwa kwenye
mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Protea Court Yard Seaview jijini Dar
es Salaam. Kutoka kulia ni Joe Mgaya, Dk.Fred Limbanga, Mkurugenzi wa
Mabibo, Benedicta Rugemalira na .Dk. Sima Rugarabamu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Wadau wa sekta ya
afya pamoja na maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye mkutano huo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Maghara wa Mabibo Beer, Boniface. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akiwa kwenye mkutano huo. Kushoto ni Dk. Fred Limbanga na mmoja wa Wakurugenzi, Respicius Didace.
Dk. Sima Rugarabamu (kulia) wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), akisisitiza jambo katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment