TANGAZO


Thursday, August 7, 2014

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yavunja nyumba kwenye kiwanja kilichoporwa Mbezi Beach

Nyumba zilizokuwa ndani ya uzio huu ndizo zilizovunjwa kwa amri ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wakili wa nyumba zilizokuwa kwenye uzio wa kitalu namba 314, Emmanuel Muga (kushoto), akizungumza na Maofisa wa Polisi kwa ajili ya kuweka zuio la kupinga kuvunjwa kwa nyumba hizo zilizokuwemo kwenye uzio (nyuma yao), wakati wa zoezi hilo leo.
Wakili Emmanuel Muga (kushoto), akiendelea kuzungumza na Maofisa wa Polisi kwa ajili ya kuzuia uvunjaji wa nyumba hizo.
Wakili Emmanuel Muga (kushoto), akimuonesha Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya (kulia), moja ya nyaraka za Mahakama, ili nyumba hizo zisivunjwe.
Wakili Emmanuel Muga (kushoto), akimuonesha Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya (kulia), moja ya nyaraka zilizotolewa na Mahakama, ili nyumba hizo zisivunjwe.
Maofisa wa Polisi wakiwa na gari lao, wakiwa katika sehemu hiyo kwa ajili ya kutoa ulinzi wakati wa uvunjwaji wa nyumba hizo leo.
Maofisa wa Polisi wakiwa kwenye gari lao, huku kijiko cha Manispaa ya Kinondoni kikipita tayari kwenda kuvunja nyumba zilizokuwa kwenye kiwanja namba 314.
Wananchi wakiwa karibu, wakiangalia maendeleo ya uvunjaji wa nyumba hizo. 
Hizi ni baadhi tu ya nyumba hizo, nne zilivyokuwa zikionekana kabla ya kuvunjwa leo asubuhi, Mbezi Beacha, jijini Dar es Salaam.
Kijiko cha Manispaa ya Kinondoni kikiendelea kuvunja ukuta wa nyumba hiyo, wakati wa kuvunja nyumba hizo.
Kijiko cha Manispaa ya Kinondoni, kikiwa tayari kwa ajili ya kuvunja nyumba hizo.
Kijiko cha Manispaa ya Kinondoni kikivunja ukuta wa kiwanja hicho, kabla ya kuvunja nyumba nne zilizokuwa zimejengwa ndani yake.
Kijiko cha Manispaa ya Kinondoni, kikivunja kwa amri ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, moja ya nyumba nne, zilizokuwa zimejengwa isivyo halali kwenye kiwanja namba 314, kinachomilikiwa na moja ya familia iliyokuwa imeporwa kiwanja hicho, maeneo ya Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam leo. 
Askari wa kutuliza ghasia, wakilinda wakati wa uvunjwaji wa nyumba hizo, kwenye kiwanja namb 314, Mbezi Beach jijini jana.
Kijiko cha Manispaa ya Kinondoni, kikivunja kwa amri ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, moja ya nyumba nne, zilizokuwa zimejengwa isivyo halali kwenye kiwanja namba 314, kinachomilikiwa na moja ya familia iliyokuwa imeporwa kiwanja hicho, maeneo ya Mbezi Beach, Dar es Salaam leo.
Mmiliki wa kiwanja namba 314, Janeth Mwaikambo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati nyumba zilizojengwa kwenye kiwanja chake hicho, zilipokuwa zikivunjwa kwa amri ya Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbezi Beach, Dar es Salaam leo.
Kijiko cha Manispaa ya Kinondoni, kikivunja kwa amri ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, moja ya nyumba nne, zilizokuwa zimejengwa isivyo halali kwenye kiwanja namba 314, kinachomilikiwa na moja ya familia iliyokuwa imeporwa kiwanja hicho, ya Janeth Mwaikambo, maeneo ya Mbezi Beach, Dar es Salaam leo. 
Mhandisi wa Manispaa ya Ilala, aliyesimamia uvunjwaji wa nyumba hizo, kwenye kiwanja namba 314, Baraka Mkuya, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la uvunjaji wa nyumba hizo leo.

Na Mwandishi wetu

WIZARA ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, leo imevunja nyumba nne za Mchungani Getrude Lwakatare zinazodaiwa kujengwa kinyume cha sheria katika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Nyumba hizo, zilibomolewa huku baadhi ya watu waliokuwa eneo hilo, kabla ya zoezi hilo kufanyika kwa zaidi ya saa mbili, wakisikika wakisema kuwa kutokana na nyumba hizo, kumilikiwa na kigogo si rahisi kuvunjwa.

Ndoto hizo kadri muda ulivyozidi kusonga mbele zilianza kuyeyuka baada ya tingatinga la Manispaa ya Kinondoni kufika saa tano na kuanza shughuli hiyo, ambayo ilivuta hisia za watu wengi.

Kuvunjwa kwa nyumba hizo, kulitokana kuwepo kwa madai ya Mchungaji Lwakatare kuvamia eneo hilo, lililokuwa likimilikiwa na Janeth Kiwia Mwaikambo, baada ya kulinunua kutoka kwa Alexander Kristonia miaka kadhaa iliyopita.


Kiwia akizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo, alisema kuwa alilimiki tangu mwaka 2010, baada ya kununua kutoka kwa mtu anayedaiwa kuwa ni shemeji yake, aliyemtaja kwa jina la Kristonia.
"Nilikuwa nikimiliki eneo hili kwa muda mrefu, lakini ilipofika mwaka 2010, nililinunua rasmi na kuanza ujenzi kidogo kigogo nyumba ilipofika kwenye rinta nilikwenda nje ya nchi, nikiwa huko, nikapigiwa simu kuwa nyumba imevunjwa na imejengwa ukuta," alisema.
Alifafanua zaidi kuwa akiwa huko, aliomba suala hilo, litolewe taarifa kituo cha polisi, hali iliyosaidia kukamatwa walinzi waliokuwa wakilinda eneo hilo na aliporejea akaendelea kusimamia suala hilo, ingawa lilijawa na wingu zito.

Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo kampuni ya Homec Advovacates kwa ajili ya kumsaidia kuendesha kesi hiyo, ambayo ilionekana wazi kumuendea kombo kutokana na kukaliwa na kigogo.

Mmoja wa mawakili wa kampuni hiyo, Howard Msechu alisema kutokana kesi hiyo kufika mahakamani na kutolewa stop order ya kutoendelezwa lakini amri hiyo ilivunjwa.

Alifafanua kuwa baada ya amri hiyo kuvunjwa kampuni yake iliamua kuiandikia barua Wizara ya Ardhi ili iruhusu nyumba zilizojengwa kwa kukaidi amri ya mahakama zivunjwe na waliokaidi wachukuliwe hatua.

"Nashukuru baada ya kuiandikia barua Wizara ya Ardhi, kuwa nyumba zilizojengwa katika kiwanja namba 314 chenye hati namba 23856, mjenzi wake alikaidi amri ya mahakama kwa kuendeleza eneo kinyume na taratibu, leo imechukua hatua ya kuzivunja.

"Hilo ni jambo jema kwa maana imeonesha kuwa haki ya mtu haiwezi kupokwa kutokana na uwezo au wadhifa wa mtu naamini baada ya tukio hili, wananchi watarudisha imani kwa Wizara ambayo awali ilionekana kama haiko kwa watu wa hali ya chini," alisema.

Awali kabla ya mchakato huo, kuanza wakili anaemtetea mama Lwakatere, Emmanuel Muga alifika na kudai kutaka kuzidia amari hiyo iliyopewa meno na Wizara ya Ardhi bila mafanikio na wakati zoezi likianza alitokomea kusikojulikana.

"Katika hatua nyingine, wakati waandishi wakiendelea na kazi alianza kuwatolea maneno ya ukali akidai kuwa hawapaswi kuwa katika eneo hilo, kutokana na kesi kuwa mahakamani na hayo ni mambo binafsi na kuahidi kwenda katika Ofisi za waandishi hao kushtaki," alisema.
Pia Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, aliyekuwa akisimamia zoezi hilo, Baraka Mkuya alisema kuwa Wizara imeamua kuchukua hatua hiyo kutokana na Mama Lakwatare kutokuwa na hati za kumiliki eneo hilo.

Alifafanua kuwa wakati akianza ujenzi huo, hakupeleka taarifa katika manispaa hiyo, kama taratibu zinavyomtaka na ilipogundulika kuwa anafanya ujenzi, alipotakiwa kufika, hakufanya hivyo.


Awali kabla ya mchakato huo kuanza baadhi ya waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo, walianza kuingiwa na hofu, wakiamini wanaweza kushambuliwa.

Kwa maana nyumba hiyo ilionekana kuimarika kiulinzi wa kampuni ya Kiwango Security na mlinzi aliyekuwa ndani ya uzio alikuwa ameshika silaha ya moto na kuwapa hofu kubwa waandushi hao.
Ilipofika saa sita na dakika tano gari la polisi lenye namba PT 1686, lilifika, likiwa na askali 12 wakiwa na mabomu ya kutoa machozi na silaha za moto, wakiongozwa na Afande, Emmanuel Tille.
Baada ya polisi hao, kufika eneo hilo na kuimarisha ulinzi na kuondoa hofu kwa waandishi, katapila la Manispaa ya Kinondoni lilifika saa sita na dakika 12 na kuanza shughuli ya kuvunja nyumba nne zilizoko eneo hilo na kuhitimisha zoezi hilo saa 8:30.

Baadhi ya watu waliohojiwa, walisema kuwa ufalme wa watu wenye fedha kudhulumu wasiokuwa na fedha siku chache utapototea na kuipongeza Wizara ya Ardhi kwa hatua hiyo.

Mchungaji Lwakwatere hakuwepo wakati zoezi hilo likiendelea akiaminika kuwa yuko mkoani Dodoma katika vikao vya Bunge la Katiba linaloendelea na alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia suala hilo, hakuweza kupatikana .

No comments:

Post a Comment