Waziri
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akifungua mkutano wa 30
wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika
(PTA), ulioandaliwa na benki hiyo leo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira na kulia ni Rais na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika
(PTA), Admassu Tadesse.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akifungua mkutano wa 30 wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA), ulioandaliwa na benki hiyo leo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira na kulia ni Rais na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA), Admassu Tadesse.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum ambaye yupo nje ya nchi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 30 wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwaA frika (PTA), iliyoandaliwa na benki hiyo leo, jijini Dar es Salaam.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwaAfrika (PTA),
Admassu Tadesse akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa benki hiyo, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
30
wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika
(PTA), leo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA), wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano wa 30 wa mwaka wa benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA), wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano wa 30 wa mwaka wa benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO
Na
Lorietha Laurence, Maelezo
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amefungua rasmi mkutano wa 30 wa
mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki chini ya udhamini wa Benki ya PTA leo jijini
Dar es Salaam.
Mhe. Pinda amewasihi
washiriki wa mkutano huo wasiishie tu kushiriki katika mkutano bali pia
wapatapo nafasi waweze kutembelea sehemu mbalimbali nchini ikiwenmo mbuga za
wanayama na vivutio vingine kwa kuwa Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana katika
sekta ya Utalii.
“kwa niaba ya Serikali ya
Tanzania nimefurahi sana kwa kutupatia nafasi hii ya kuwa wenyenji wa mkutano
huu hivyo tunawakaribisha washiriki waweze kutembelea vivutio mbalimbali
vilivyomo nchini kwetu pale wapatapo nafasi” alisema Mhe.Pinda
Aliongeza kusema benki
ya PTA imesaidia katika kukuza na kuinua
uchumi wa Afrika kwa nchi washiriki na kwa kufanya hivyo imeongeza chachu ya
kuwepo mshikamano na mahusiano mazuri baina ya nchi hizo.
Aidha Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Uratibu na Uhusiano Mhe.Steven Wassira kwa niaba ya Waziri wa Fedha
Mhe. Saada Mkuya ameshukur kwa fursa ya kusimamia mkutano huo wenye lengo la kujadili
mambo ya kibenki na uchumi kwa nchi washiriki.
“kupitia mkutano huu
Tanzania inapata fursa ya kuweza kujadili mambo mbalimbali yanahusu maendeleo
na namna ya kujikwamua kutoka katika umaskini tunaishukuru Benki ya PTA kwa
kutupa nafasi hii na tunawakaribisha tena kwa wakati mwingine”alisema Mhe.
Wassira.
Naye Rais na Mtendaji
Mkuu wa Benki ya PTA, Admassu Tadesse ameishukuru serikali ya Tanzania kwa
kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
Benki ya PTA inatoa
huduma zake kwa nchi wanachama ikiwa na
lengo la kuwa Taasisi ya kifedha inayoongoza
Mashariki na Kusini mwa Afrika katika utoaji wa huduma za kibenki ambapo
mwaka huu imetimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1985.
No comments:
Post a Comment