TANGAZO


Thursday, August 28, 2014

Vijana wapewa changamoto ya kutumia uzazi wa mpango

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sabasaba Bw.Ibrahim  Mwita akizungumza na Vijana wa kikundi cha Bank Club wakati wakati wa Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia  Kituo cha Vijana YAM  kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba  kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”Kulia ni Afisa Vijana wa UMATI Bibi. Upendo Daud.
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Sabasaba wakipata maelezo kuhusu afya ya uzazi wa mpango kutoka kwa waelimisha rika wa UMATI walipokuwa katika Jamvi la Vijana lilioshirikisha Kikundi cha Vijana cha Benki Club kutoka  Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni.
 Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Sabasaba wakipata maelezo kuhusu afya ya uzazi wa mpango kutoka kwa waelimisha rika wa UMATI walipokuwa katika Jamvi la Vijana lilioshirikisha Kikundi cha Vijana cha Benki Club kutoka  Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni.
Ofisa Vijana wa UMATI kutoka Temeke Bibi. Upendo Daud akimkabidhi zawadi ya machapisho kuhusu Afya ya uzazi wa mpango Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba  ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika Jamvi la Vijana lililofanyika katika mtaa wake. Jamvi la Vijana ni program ambayo  inaendeshwa na UMATI kupitia  Kituo cha Vijana YAM  kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba  kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
Mmoja wa washereheshaji katika Jamvi la Vijana akimkabidhi mtoto Shani Rajab zawadi ya Jarida la Fema baada ya kujibu swali kuhusu uzazi wa mpango katika Jamvi la Vijana lililofanyika katika mtaa wa Sabasaba na kuhusisha Kikundi cha Vijana cha Benki Club kutoka kata ya Mtoni  iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni. Jamvi la Vijana ni program ambayo  inaendeshwa na UMATI kupitia  Kituo cha Vijana YAM  kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba  kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
Baadhi ya wananchi wakifuatilia igizo kutoka kwa Kikundi cha Vijana cha Benki Club (hakipo pichani) wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika mapema hivi karibuni katika mtaa wa Sabasaba  uliopo katika Kata ya Mtoni  Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Jamvi la Vijana ni program ambayo  inaendeshwa na UMATI kupitia  Kituo cha Vijana YAM  kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba  kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
Baadhi ya waigizaji wa Kikundi cha Vijana cha Benki Club wakiigiza kuhusu namna ambavyo mwanaume anamshinikiza mke wake abebe mimba mara baada ya miezi michache tokea ajifungue,igizo hilo lilionyeshwa  wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika mapema hivi karibuni katika mtaa wa Sabasaba  kata ya Mtoni  iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Jamvi la Vijana ni program ambayo  inaendeshwa na UMATI kupitia  Kituo cha Vijana YAM  kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba  kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sabasaba uliopo katika Kata ya Mtoni Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Bw. Ibrahim Mwita (waliosimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kikundi cha Vijana cha Benki Club wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni. (Picha zote na Frank Shija, MAELEZO)

Na Frank Shija, MAELEZO
VIJANA wameaswa kutoona haya katika kujifunza na kuzingatia elimu mbalimbali kuhusiana na  Afya zao ikiwemo  uzazi wa mpango na  na maambukizi ya Ukimwi.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Sabasaba uliopo katika Kata ya Mtoni Manispaa ya Temeke Bw. Ibrahim Mwita wakati akiongea na wakazi wa mtaa huo wakati wa Jamvi la Vijana lililokuwa lililohusisha Vijana mbalimbali kutoka mtaa huu.

Mwita alisema kuwa ni vyema vijana wakajitokeza kwa wingi katika kujifunza uzazi wa mpango na kupia afya zao hili waweze kuwa na mueleke sahihi katika kujililanda na maaradhi ikiwemo Ukimwi.
Aidha Mwenyekiti huyo ameipongeza UMATI kwa kupeleka program hiyo ya Jamvi la Vijana katika mtaa wake na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano pale panapohitajika ili kueneza zaidi elimu hiyo muhimu kwa jamii.

“Nawapongeza ndugu zangu wa UMATI kwani hii inaonyesha kabisa fedha mnazopata kutoka kwa wafadhili mnazitumia kweli kwa manufaa ya jamii hii ni faraja kubwa sana kwetu ata nikiambiwa nichangie nitakuwa mstari wa mbele”. Alisema Mwita.

Kwa upande wake Afisa Vijana wa UMATI kutoka Manispaa ya Temeke Bibi. Upendo Daud amesema kuwa wao kama wadau wa katika sekta ya afya ni wajibu wao kutumia fursa waliyonayo kutoa elimu kwa jamii juu ya afya ya uzazi wa mpango na malezi kwa  ujumla.
Upendo aliongeza kuwa kupitia program ya Jamvi la Vijana vijana wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kuhusu uzazi wa mpango, VVU na pia wanapata fursa ya kupima afya zao bila gharama yoyote ile.

Naye Mwenyekiti wa Kikundi Cha  Vijana cha Benki Club Bw. Mohamed Kipati amesema kuwa imekuwa faraja kwao kwa kufikiwa na Jamvi la Vijana katika mtaa wao kwa kuwa itawaongezea morali ya kuendelea na program zao za kutoa elimu kwa jamii inayowazunguka.

Mohamed aliongeza kuwa kupitia Jamvi hilo wameweza kuongeza maarifa na mbinu za kusamba ujumbe wa kuhamasisha vijana kushiriki katika afya ya uzazi wa mpango na malezo.


Jamvi la Vijana ni program inayoendeshwa na Chama cha Malezi na Afya ya Uzazi Tanzania (UMATI)  kupitia Kituo cha Vijana cha YAM na Malezi Youth Theatre kutoka Manispaa ya Temeke.

 Jamvi hilo la  Vijana lililofanyika katika mtaa wa Sabasaba ulipo Kata ya Mtoni Manispaa ya Temeke lilibeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki juu ya kutumia uzazi wa mpango?”

No comments:

Post a Comment