Balozi wa amani Tanzania Risasi Mwaulanga
Na
Rose Masaka-MAELEZO
UKAWA waombwa kukubali
maoni ya watanzania walio wengi ya kuheshimu pesa za walipa kodi kwa kurudi
bungeni na kupingana kwa hoja kwani hoja zao zikiwa za uhakika hazitapingwa
bali kanuni na taratibu zinazoendesha bunge zitafuatwa badala ya kuendelea
kulalamika katika majukwaa ya kisiasa.
Kauli hiyo imetolewa na
Balozi wa amani Tanzania Risasi Mwaulanga alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari katika ukumbi wa habari maelezo leo jijijni Dar es Salaam.
“Nawaomba UKAWA warudi
bungeni ili tuweze kupata katiba mpya itayoyokidhi changamoto za watanzania
wote na sio masuala ya vyama vya kisiasa na maslahi binafsi kwani vyama hiyvo
vinaweza kutoweka wakati wowote na nchi ikabaki palepale”.Alisema Mwaulanga.
Aidha Mwaulanga anaiomba
iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya jaji Warioba, viongozi wa dini, na
asasi za kiraia kuendelea na jitihada za kuitaka UKAWA kurejea Bungeni ili
kurahisisisha upatikanaji wa Katiba mpya yenye maslahi mapana kwa ummma kuliko
ya kisiasa.
Balozi huyo wa amani
amesema kuwa kauli za vitisho na uvunjifu wa amani unapaswa kupigiwa kelele na
kulaniwa na kila mwanademokrasia duniani katika kipindi hiki cha kuandaa Katiba
mpya ili wajumbe waweze kuwa huru wakati wa kutoa maoni.
Tanzania ni nchi ya
amani,umoja, upendo na maelewano na siyo nchi ya vita,chuki na mafarakano hivyo
watanzania tunapaswa kutambua ni Katiba gani tunayoitaka na kuwa na mtazamo
sahihi na maamuzi bora.


No comments:
Post a Comment