Rais wa Ufaransa Francois
Hollande ametangaza kuwa taifa lake litawahami wapiganaji WaKurdi
iliwakabiliane na wapiganaji wa Islamic State kaskazini mwa Iraq.
Kulingana na taarifa katika vyombo vya habari
vya Ufaransa ,Rais Hollande amepata ruhusa kutoka kwa mamlaka nchini
Iraq kuendelea mbele na mpango huo mahsusi wa kuidhibiti Islamic State.Wapiganaji wa kikurdi wamekuwa wakipiganaji na wapiganaji wa wanamgambo wa Islamic state ambao wameunda himaya yao kaskazini mwa Iraq pamoja na sehemu za Syria.
Mapigano hayo yamesababisha kutokea kwa maelfu ya wakimbizi katika maeneo hayo Kaskazini mwa Iraq.
Hatua hiyo ya bwana Hollande inafwatia ombi la wakuu wa jimbo la Kurdistan la kuitisha msaada wa kijeshi.
Mapema leo serikali ya Marekani ilituma washauri 130 wa kijeshi katika jimbo la Kurdistan.
Marekani tayari inaendelea na kampeini ya vita vya hewani dhidi ya IS katika jitihada za kuwazuia wasitawale eneo zima la Kaskazini mwa Iraq.
Kiongozi wa waKurudi Massoud Barzani, ameomba msaada wa kijeshi baada ya Islamic state kutwaa miji kadhaa karibu na jimbo la Kurdistan.
No comments:
Post a Comment