TANZIA
![]() |
| Marehemu Bi. Hamisa Mahanyu |
Shirikisho la Michezo ya
Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) linasikitika kutangaza kifo cha
Mwanamichezo Bi. Hamisa Mahanyu aliyekuwa mchezaji wa timu ya kamba ya wanawake
ya Ofisi ya Rais, IKULU kilichotokea kwa ajali ya gari tarehe 04 Agosti, 2014
eneo la Sayansi – Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Marehemu
unasafirishwa leo tarehe 05 Agosti, 2014 kwenda Lushoto kwa mazishi.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MPENDWA WETU HAMISA MAHANYU MAHALI PEMA
PEPONI AMINA
Imetolewa leo tarehe 05 Agosti, 2014
Moshi
Makuka
KAIMU
KATIBU MKUU - SHIMIWI


No comments:
Post a Comment