TANGAZO


Sunday, August 24, 2014

Serengeti Fiesta yaacha gumzoTanga

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Khadija, akikonga nyoyo za mashabiki walioingia katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga  mwishoni mwa wiki.
Umati wa watu uliofurika kaika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kupata burudani safi wakati wa tamasha la Serengei fiesta mwishoni mwa wiki.
Msanii wa bongo fleva, Jux, akiiimba katika tamasha la Serengeti fiesta mjini Tanga mwishoni mwa wiki.
Staa wa  muziki wa bongo fleva , Young Killer, akiimba katika tamasha la Serengeti fiesta mjini Tanga mwishoni mwa wiki. 
Mkuu wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego (kulia), akimkabidhi kiongozi wa kundi la Ice Cream, Hamisi Kanda, (kushoto)  shilingi milioni moja ,baada ya kundi hilo kuibuka mshindi wa shindano la Super Dansi la Serengeti Fiesta.
Wasanii wa Kundi la Ice Cream wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni moja baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Super Dansi la Serengeti Fiesta.
Mkali wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya  Mr. Blue akifanya vitu vyake katika  onyesho la Serengeti fiesta lililofanyika juzi mjini Tanga.
Mkali wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya  Mr. Blue akifanya vitu vyake katika  onyesho la Serengeti fiesta lililofanyika juzi mjini Tanga.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya , Linah akiburudisha wapenzi wa muziki huo jana katika onyesho la Serengeti fiesta lililofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani Mjini Tanga mwishoni mwa wiki
Mkali  wa bongo fleva , Ally Kiba akikonga nyoyo za mashabiki wa kati wa onyesho la Sereneti fiesta lililofanyika katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga mwishoi mwa wiki.
Msanii Ney wa mitego akiwapagawisha mashabiki wa miondoko hiyo katika tamasha  la  Serengeti fiesta lililofanyika katika  uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga mwishoni mwa wiki.
Wasanii Ney wa mitego na Stamina wakimiliki jukwaa la wakati wa atamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga mwishoni mwa wiki.
Msanii Ney wa mitego akiwapagawisha mashabiki wa miondoko hiyo katika tamasha  la  Serengeti fiesta lililofanyika katika  uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga mwishoni mwa wiki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya , Roma Mkatoliki ambaye pia ni mwenyeji wa Mkoa wa Tanga , akionyesha makali yake wakati wa tamasha  la Serengeti fiesta lililofanyika katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga mwishoni mwa wiki
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoloki ambaye pia ni mwenyeji wa Mkoa wa Tanga , akikonga nyoyo za maelfu ya wakazi wa mkoa huo na maeneo jirani wakati wa tamasha la Serengeti fiesta katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga mwishoni mwa wiki
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya , Roma Mkatoloki ambaye pia ni mwenyeji wa Mkoa wa Tanga , akikonga nyoyo za maelfu ya wakazi wa mkoa huo na maeneo jirani wakati wa tamasha la Serengeti fiesta katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga mwishoni mwa wiki


SIKU chache baada ya Serengeti fiesta kutoa burudani ya kufa mtu katika uwanja wa Kahama,  historia imejirudia tena Jijini Tanga pale Kampuni ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Premium Serengeti walipopeleka kundi la wasanii wapatao 15 na kutoa burudani katika uwanja wa Mkwakwani.


Maelfu ya mashabiki jijini hapo walijitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii wao vipenzi. 

Masaa kadhaa kabla ya burudani hiyo kuanza, uwanja wa Mkwakwani ulikuwa umefurika mashabiki kutoka vitongoji mbalimbali vinavyo lizunguka jiji hilo.


Huku burudani ikiendelea kutolewa, tiketi pia ziliendelea kuuzwa mpaka majira ya saa saba usiku. 
Ilipofika majira ya saa tisa usiku wadhamini wa burudani hiyo waliruhusu mageti yafunguliwe ili mamia ya mashabiki waliokuwa nje waingie ndani ya uwanja kujumuika na wenzao. 


“Kila msanii amepanda jukwaani akiwa na lengo moja tu…kutoa burudani na kuhakikisha amewaridhisha mashabiki wake,  jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limewapelekea wasanii kutoa  burudani ya kufa mtu,” alisema Ali Kiba dakika chache kabla hajapanda jukwaani.


Akiwa jukwaani, aliudhihirishia umati uliojitokeza uwanjani hapo kwamba yeye bado ni gwiji la muziki Afrika Mashariki na Kati.

Umahiri wake katika kucheza na sauti kulifanya mashabiki wake kupagawa na kupiga kelele zilizo sambaa uwanjani hapo. 

Walio wengi hawakutamani amalize mapema kwani kila alipoonesha dalili za kumaliza mashabiki wake walipiga kelele kuonesha ishara ya kutaka aendelee kuimba zaidi.


Shangwe zilirindima zaidi, pale mototo na mzaliwa wa Tanga, Roma Mkatoliki alipopanda jukwaani kutoa burudani.


Roma alionekana akiwa na nguvu na ari ya kutoa burudani kwa mashabiki wake kama alivyo ahidi siku chache zilizopita.


Akiwa jukwaani aliruhusu mashabiki wake waimbe pamoja naye ikiwa ni ishara ya kusambaza upendo kwa kila aliyejitokeza uwanjani hapo.

Wasanii wengine waliotoa burudani katika uwanja wa Mkwakwani ni pamoja na Recho, Chege na Temba, Ali Kiba, Ney wa Mitego, Stamina, Jux, Linah, Vanessa Mdee, Mr Blue,  Mkubwa na Wanae, Ommy Dimpoz, Barnaba, Young Killer and  Madee.

“kwa mwaka huu, Serengeti Fiesta Tanga imepokelewa kwa ari ya juu sana. 
Wanatanga wamejitokeza kwa wingi sana kutuunga mkono. 

Ninatumia fursa hii kuwashukuru wana-Tanga kwa kuonesha upendo wao kwa Serengeti Fiesta,” alisema Meneja Chapa wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney.


Serengeti Fiesta Tanga pia iliambatana na burudani mbalimbali kama Serenegeti Soccer Bonanza na Dance la Fiesta.


Baada ya Tanga, burudani la fiesta litaelekea Musoma, Shinyanga, Kigoma,  Tabora, Singida, Dodoma, Moshi, Arusha, Mtwara na baadaye kumalizika jijini Dar es Salaam October 18 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment