Mkurugenzi na Katibu Mtendaji wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania (TSNP), Alphonce Lusako, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mwenendo wa Mchakato wa Katiba, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi na Katibu Mtendaji wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania (TSNP), Alphonce Lusako (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza nao, kuhusu mwenendo wa Mchakato wa Katiba, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kwenye mkutano na Uongozi wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania (TSNP), wakati ulipokuwa ukizungumza nao, kuhusu mwenendo wa Mchakato wa Katiba, Dar es Salaam leo.
Na Rose Masaka
Na Rose Masaka
MTANDAO wa wanafunzi nchini (TSNP) Umetoa tamko dhidi ya mwenendo
wa mchakato wa kupata Katiba mpya ya Tanzania.
Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa wanafunzi Bwana Alphonce Lusako
ametoa tamko hilo katika mkutano ulioudhuriwa na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam.
Lusako ametoa ombi kwa vyama vyote vya siasa kurudi bungeni
na kufanya maridhiano ili tuweze kupata katiba mpya ambayo itasaidia kuokoa
mabilioni ya fedha za watanzania ambazo zimekwisha tumika katika mchakato wa
kutafuta katiba mpya.
“Tunawaomba CCM, UKAWA, TANZANIA ONE na wajumbe wa Bunge Maaalum
la Katiba kujua kuwa kushindwa kwa mchakato huu siyo kushindwa kwa kwa chama chochote ila ni kushindwa kwa Watanzania,”alisema
Lusako.
Viongozi wa mtandao wa wanafunzi nchini, umewaomba UKAWA, CCM
na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wafikie muafaka na watambue kuwa sheria
kuu ya wao ndani ya bunge ni kuboresha Katiba ya wananchi na siyo kupindua
maamuzi ya wananchi.
Wajumbe wa Bunge Maalum
la Katiba wanatakiwa wajue kuwa hawapo
kwa ajili ya kutafuta na kutambua mshindi na mshindwa, bali upo kwa ajili ya
ushindi wa watanzania ambao pesa zao nyingi zimetumika.
Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa, mchakato haupo kwa ajili ya
kutambua nani anamsimamo huu na msimamo ule,bali upo kwa ajili ya kutambua
msimamo wa watanzania juu ya namna gani taifa lao litaongozwa na katiba
iliyotokana na mawazo yao.
Mtandao wa wanafunzi nchini uliitisha kongamano rasmi la
wanafunzi wa Vyuo Vikuu na sekondari kwa ajili ya kujadili mchakato mzima wa
kupata Katiba mpya ndani ya Taifa letu ambao uliwapa wanafunzi fursa ya kupaza
sauti zao juu ya mchakato mzima wa katiba.

jamii iko pamoja nanyi
ReplyDelete