Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jaap Frederiks akitoa hotuba yake kwa wanafunzi (Watanzania) waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika Agosti 21, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay, jijini Dar es Salaam
Wanafunzi wa Kitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika Vyuo mbalimbali nchini Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao, iliyofanyika Agosti 21, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Kitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika Vyuo mbalimbali nchini Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao, iliyofanyika Agosti 21, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga-MAELEZO-DSM)
Na Benedict Liwenga-MAELEZO
KATIBU Mkuu Kiongozi,
Ombeni Sefue amehudhuria hafla ya kuwaaga wanafunzi waliopata udhamini kwenda kusoma nchini Uholanzi katika sekta mbalimbali zikiwemo za mafuta na gesi,
miundombinu, kilimo, maji, afya pamoja na Maendeleo ya sekta binafsi.
Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa Balozi wa Uholanzi eneo la
Oysterbay, jijini Dar es Salaam
ambapo Katibu Kiongozi ndiye alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo.
Katibu Kiongozi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa
program iliyoanzishwa na nchi ya Uholanzi wa kuwasaidia Watanzania kupata ufadhili kamili wa kwenda kusoma masomo mbalimbali nchini humo na ujuzi wanaoupata uweze kulisaidia Taifa pamoja na Watanzania wengine kwa ujumla.
“Ninaamini kuwa wanafunzi hawa waliopata ufadhili huu wa masomo mbalimbali nchini Uholanzi watapata fursa kubwa ya kusomea
mambo mbalimbali na ujuzi huu hawatakaa nao wenyewe binafsi,
bali watalisaidia taifa na Watanzania wengine,
hivyo, wajenge moyo huo, wa kutokuwa wabinafsi”. Alisema Sefue.
Naye Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.
Jaap Frederiks amesema kuwa amefurahi kwa muamko mkubwa wa Watanzania wengi wa kuomba nafasi za masomo nchini kwake na amewaasa wengine kuiga mfano huo, kwani nchi yake itaendelea na programu hiyo, kulingana na bajeti pamoja na wataalamu waliopo nchini Uholanzi.
“Nchi yangu inatoa fursa ya masomo kwa Watanzania kwenda kusoma lakini tunaangalia maeneo ambayo
tuna wataalamu ambao wanaweza kuwasaidia Watanzania kuwapa elimu,
hivyo ni jukumu lao wenyewe Watanzania kuaamua maeneo gani ya kusomea pamoja na kozi wazipendezo”.
Alisema Frederiks.
Katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita,
zaidi ya Watanzania elfu tano wamepata udhamini wa kusoma katika sekta mbalimbali, zikiwemo Utawala wa Fedha,
Uhandisi, Miundombinu, Kilimo, Afya, Elimu na Utawala ambapo hii inaifanya Tanzania
kuwa moja ya wanufaikaji wakubwa duniani wa programu hii ya udhamini wa masomo, ambapo wengi wa Watanzania waliopata nafasi hizi wameshika nyadhifa muhimu katika jamii ya
Tanzania kitua mbacho kinaendeleza ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment