Hatimaye mshambulzi wa Colombia
James Rodriguez aliyeduwaza ulimwengu kwa kufunga mabao mengi zaidi
katika kombe la dunia lililokamilika huko Brazil mwezi uliopita amepokea
tuzo lake la mfungaji mabao mengi '' Golden Boot''.
Rodriguez ambaye aliyetikisa wavu mara 6 huko
Brazil sasa anakibarua cha kutafuta namba huko Real Madrid dhidi ya
wakinzani wenye haiba yake kama mchezaji bora msimu huu Christiano
Ronaldo.Rodriguez alinunuliwa na mabingwa hao wa kombe la mabingwa barani ulaya kutoka Monaco kwa pauni milioni 71.
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23 alisema kuwa anamatumaini makubwa ya kutamba Santiago Bernabéu.
Colombia ilitegemea mabao yake sita katika mechi 5 kufuzu kwa hatua ya robo fainali kabla ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya wenyeji Brazil.
No comments:
Post a Comment