Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Mario Balotelli anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake uliogharimu kiasi cha pauni milioni 16 kuelekea Anfield akitokea AC Milan hii leo.
Winga wa zamani wa Everton Kevin Kilbane ana matumaini kuwa Balotelli ataleta mabadiliko ya haraka sana ambayo Liverpool inahitaji, chini ya kocha Brendan Rodgers.
Hata hivyo taratibu za kuangusha wino hazitafanyika kwa haraka ili kumuwezesha kukabiliana na waajiri wake wa zamani, ambapo hii leo patachimbika katika uwanja wa Etihad Liverpool itakapovaana na Manchester city.
Baloteli ameichezea kwa mafanikio Manchester City kwa miaka miwili na nusu hata hivyo amekuwa akikemewa mara kadhaa kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.
Pamoja na hayo Liverpool inategemea mazuri kutoka kwake huku Rodgers akitarajiwa kumuweka Balotelli kwenye mstari wakati wote atakapoitumikia Liverpool.
No comments:
Post a Comment