TANGAZO


Friday, August 8, 2014

Ajali yatokea maeneo ya Afrikana, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo mchana


Gari aina ya Nissan Hard Body yenye Namba za Usajili T 524 ALW likiwa limetupwa mtaroni na trela la lori (halipo pichani),  ambalo lililigonga gari hilo na kutumbukia mtaroni eneo la Afrikana Mbezi Beach Mchana wa leo. Katika Ajali hiyo iliyohusisha Lori na gari aina ya Nissan Hard Body hakuna mtu yoyote aliyepoteza Maisha.
Wananchi wakisaidia Kulifunga minyororo gari aina ya Nissan Hard Body ambayo imetumbukia mtaroni mara baada ya Kugongwa na trela la lori (halipo pichani) mchana wa leo katika Eneo la Mbezi Afrikana.
Wananchi wakisaidia kuligeuza gari ndogo aina ya Nissan Hard Body iliyotumbukia mtaroni eneo la Afrikana Mbezi Beach mara baada ya Kugongwa na trela la lori (halipo pichani) mchana wa leo, katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha. (Picha zote na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog)

No comments:

Post a Comment