TANGAZO


Friday, August 29, 2014

4 hatiani kwa jaribio la kumuua Nyamwasa






Wawili kati ya sita walioshitakiwa wamefutiwa mashitaka

Wanaume wanne waliokuwa wameshitakiwa kwa kosa la jaribio la kumuua aliyekuwa jasusi wa Rwanda Generali Faustin Kayumba Nyamwasa, nchini Afrika Kusini wamepatikana na hatia ya kosa hilo.
Nyamwasa alipigwa risasi na kujeruhiwa mwezi Juni mwaka 2010 nje ya nyumba yake mjini Johannesburg. 
Washukiwa wengine wawili akiwemo aliyekuwa dereva wake Nyamwasa, walifutiwa mashitaka yao na hakimu Stanley Mkhari aliyetoa uamuzi wa kesi hiyo.
Nyamwasa alikimbilia nchini Afrika Kusini miezi kadhaa baada ya kukosana na aliyekuwa mshirika wake Rais Paul Kagame.
Sady Abdou, Hemedi Denengo Sefu, Amani Uriwani, Richard Bachisa, Hassann Nduli na Pascal Kanyandekwe, ndio wanaume sita waliokuwa wameshitakiwa kwa kupanga njama ya kumuu Nyamwasa. Wote walikanusha madai hayo.
Serikali ya Rwanda imekanusha madai ya kuhusika na jaribio la kumuua Nyamwasa.
Hukumu dhidi yao itatolewa tarehe 10 mwezi Septemba.
Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko anasema kuwa Nyamwasa alikuwa mahakamani kusikiliza kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment