Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Stima Kabikile
(katikati) akimkaribisha rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) wakati
alipofanya ziara yake ya siku moja katika Manispaa za Ilala, Kinondoni na
Temeke kwaajili ya kupata taarifa kuhusu kodi za majengo na utendaji kazi wa
wataalam wanaoshughulikia masuala hayo na mbinu za kuboresha namna ya
ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia walipaji kodi.
Waziri wa Fedha, Bi Saada Mkuya akiweka saini katika kitabu
cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala kwaajili ya ziara yake ya siku moja ndani ya jiji la Dar es
salaam kwaajili ya kupata taarifa kuhusu kodi za majengo na utendaji kazi
wa wataalam wanaoshughulikia masuala hayo na mbinu za kuboresha namna ya
ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia walipaji kodi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya (kulia) Ilala
akimsomea taarifa ya makusanyo ya kodi za majengo na mikakati yake ya
kufikia malengo waliojipangia ili kuongeza mapato Mhe. Waziri wa Fedha Bi.
Saada Mkuya wakati wa ziara ya siku moja katika Manispaa za Ilala, Temeke na
Kinondoni.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya akipitia moja ya taarifa
alizopewa na uongozi wa Halmashauri wilaya ya Kiondoni wakati alipofanya ziara
yake ya siku moja ofisi hapo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty
(kulia) akimpokea Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakati alipofanya
ziara ya kikazi katika ofisi ya Manispaa hiyo jana kwaajili ya kupata taarifa
mbalimbali kuhusu makusanyo ya kodi za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri
ya kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji
kodi ambao ni wananchi.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo wakisikiliza
maelezo mazuri toka kwa Waziri wa Fedha kuhusu namna ya kuboresha makusanyo ya
kodi za majengo kwa kujikita na matumizi ya TEHAMA katika ukusanayaji wa kodi
hizo kama njia rahisi ya kuwarahisishia walipaji kodi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) akihutubia mkutano
huku akisisitiza juu ya kujikita zaidi katika kutumia TEHAMA katika kukusanya
kodi za majengo kama njia rahisi inayomrahisishia mlipaji kodi kuweza kulipa
kodi zake katika vituo vya huduma.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda
(kulia) akitoa maelezo yake kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto)
wakati wa mkutano na viongzoi wa Manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto), akiweka saini
katika kitabu cha wageni mara alipowasili ofisi za Manispaa ya Kinondoni
kwaajili ya ziara ya kikazi jana kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu
makusanyo ya kodi za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo
ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji kodi ambao ni
wananchi. Kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia), akiongozana na
viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi
ya Manispaa hiyo jana kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo ya
kodi za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo ya
ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji kodi ambao ni wananchi.
katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Bw. Yusuph Mwenda na kushoto ni
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke
Bw. Photidas Kagimbo (kulia), akisalimiana na Waziri waFedha, Mhe. Saada
Mkuya (kushoto) mara alipowasili katika ofisi za Manispaa hiyo kwa ziara ya
kikazi katika jana kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo
zikiwemo njia wanazotumia kukusanya kodi za majengo pamoja kupeana mikakati
mizuri ya kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi
walipaji kodi ambao ni wananchi.
|
Waziri wa
Fedha, Mhe. Saada Mkuya akitoa hotuba fupi yenye kuwaelekeza viongzoi wa
Manispaa ya Temeke huku akiwasisitizia kutumia mifumo ya TEHAMA katika kuleta
ufanisi ukusanyaji kodi kama njia rahisi inayowasaidia walipaji kodi kutopata
usumbufu wakati wa ulipaji.
Wajumbe
kutoka Manispaa ya Temeke wakisikiliza kwa makini maelezo yakiyotolewa na
Mkurugenzi wao (hayupo pichani) kuhusu taarifa aliyokuwa akiwasilisha jana
katika Manispaa hiyo.
Mtathmini
wa Manispaa ya Temeke Bw. Victor Ndonne (kushoto) akimuonyesha nyaraka za
makusanyo ya kodi za majengo Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (aliyekaa
katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja katika Manispaa hiyo. (Picha zote na Benedict
Liwenga)
|
WAZIRI wa Fedha Bi. Saada Mkuya amefanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ili kupata taarifa za makusanyo ya kodi za majengo ikiwa ni eneo moja kati ya maeneo sita ambayo yamepewa kipaumbele katika suala la ukusanyaji wa kodi kama vile eneo la kilimo na miundombinu.
Bi. Saada Mkuya amesema kuwa aliahidi kufanya ziara hiyo katika kikao
kilichofanyika wiki iliyopita baada ya kurudisha zoezi la ukusanyaji wa kodi za
majengo katika Serikali za Mitaa ili kuona kinachoendelea, kupata uhalisia na
changamoto zinazowakabili watendaji wote wa Manispaa ya Ilala, Kinondoni
naTemeke.
“Tumerudisha makusanyo ya kodi za majengo kwenye mitaa kwasababu
ni rahisi na wanajua nyumba zote” alisema Bi. Mkuya.
Kodi ya majengo imekuwa ni moja ya chanzo kikubwa
kinachotegemewa na Halmashauri za wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.
Serikali iliona hili mnamo mwaka 2013 na kuteua chanzo hiki kuwa mfano katika
mpango wake wa matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Kwa upande wake Mweka hazina wa Wilaya ya Ilala Bw. Stima
Kabikile amesema kuwa Halmashauri ya Illala kupitia kitengo chake cha uthamini
kwa kushirikiana na viongozi wa kata na mitaa wamejiwekea malengo ya kuyatambua
majengo 10,000 ambayo hayakuwepo katika jedwali la awali kwa kutumia njia
rahisi ya haraka ya uthamini.
“Tumeweza kubaini na kuongeza idadi ya majengo 6,820 kati ya
10,000 tuliyokadiria yenye thamani ya Shilingi bilioni 989.6 yenye tozo ya
kiasi cha shilingi trilioni 1.5 na kuweka kwenye mfumo tayari kwa malipo”. Alisema
Bw. kabikile.
Mtaalamu wa kodi za majengo Wilaya ya Ilala Bw. Joseph
Kawiche amesema kuwa kila mmiliki wa nyumba hulipa kutokana na asilimia zake
ingawa kuna baadhi ya watu ambao hawajaona umuhimu wa suala hili na kuwa
wanafichiana majina,kwa hiyo wameona ni vizuri kutumia njia mbadala ya picha
ili kuwabaibni wanaokwepa kulipa kodi.
Kwa upande wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Wilaya hiyo
Bw. Yusuph Mwenda amesema kuwa ameona umuhimu mkubwa wa kutumia Serikali za Mitaa
na kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari na vipaza sauti ili kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu kulipa kodi za majengo.
“Wenyeviti wa mitaa 171,watendaji wa Kata 34 na Watendaji wa
Mitaa 171 wanashiriki na kuainisha majengo yaliyoachwa wakati wa uthamini”. Alisema
Mwenda.
Mkurugenzi wa wilaya ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty
amesema kuwa jumla ya Shilingi bilioni 1.1 zimekwishakusanywa katika majengo
3123,aidha majengo 3120 yaliyobakia yenye wigo wa kodi bilioni 1.4 yao katika
hatua nzuri ya ulipaji.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke amesema
kuwa Halmashauri imekusanya kiasi cha shilingi milioni 165.7 kutokana na
majengo ambayo awali hayakuwepo katika daftari la majengo ambapo mapato
yanatarajiwa kuongezeka kwa hali ya juu katika mwaka huu wa fedha baada ya
majengo yote 10,000 kuthaminiwa.
Baadhi ya changamoto zinazozikabili Wilaya hizo ni pamoja na
waraka wa msamaha wa kulipa kodi ya majengo wakati sheria ipo kimya wakati
wanamiliki majengo ya makazi,kupangishana biashara ambao raia na wanajeshi wastaafu wanao,pia
shule binafsi kudai kutoa huduma wakati ada zao zipo juu, hivyo Manispaa zote
tatu zimetoa wito kwa wananchi wa Tanzania kulipa kodi kwa hiari na Serikali iweke
wazi sheria za misamaha kama zipo.
No comments:
Post a Comment