Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith
Mahenge (katikati) akiambatana na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda
cha M.M Integrated Steel Mills Ltd, Lawrence Manyama (kulia) wakati
walipowasili kwenye kiwanda hicho kwa ukaguzi.Kushoto ni Mwanasheria wa Baraza
la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) Manchare Heche.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith
Mahenge (mwenye koti la bluu) akijadili jambo na Maofisa wa Baraza la Taifa la
Hifadhi ya Mazingira (NEMC) juu ya mchanganyiko wa mabaki ya madini
yanayotumika kwenye kiwanda cha M.M Integrated Steel Mills Ltd.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith
Mahenge (kulia), akimhoji Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda cha M.M Integrated
Steel Mills Ltd, Lawrence Manyama (kulia kwake) kuhusu chemba inayopitisha
majitaka ya kiwanda hicho.Wengine ni maafisa wa wa Baraza la Taifa la Hifadhi
ya Mazingira (NEMC.
Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda cha M.M Integrated
Steel Mills Ltd, Lawrence Manyama (katikati), akitoa maelezo kuhusu kiwanda
hicho.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge na
kushoto ni Mkuu wa Biashara wa kiwanda hicho Shashikant Modi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith
Mahenge( kulia) akitoa msiamamo wa Serikali kuhusu kiwanda hicho baada ya
kukikagua.Katikati ni Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda cha M.M Integrated Steel
Mills Ltd, Lawrence Manyama na Mkuu wa Biashara wa kiwanda hicho Shashikant
Modi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge, akitoa maelekezo kwa
wamiliki wa kiwanda cha BIDCO Oil & Soap Ltd( hawapo pichani) juu ya
kusitisha kutumia magogo kama chanzo cha nishati.Aliyevaa overall ya njano ni
Msimamizi Mkuu wa kiwanda hicho David Kiawa akimsikiliza.
Meneja Mkazi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Cocacola
Kwanza, Luois Coetzee (mwenye kofia nyekundu) akimweleza jambo Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge (mwenye koti la bluu) kuhusu
tangisamaki kama kiashiria cha ubora wa majitaka yanaotibiwa na kiwanda hicho.
Meneja Mkazi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Cocacola
Kwanza, Luois Coetzee (mwenye kofia nyekundu) akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge, jinsi soda zinavyotengenezwa na kukaguliwa
kwenye kiwanda hicho.Kulia ni mfanyakazi anayekagua soda zilizotengenezwa kabla
ya kupakiwa. (Picha
zote na Hussein Makame-MAELEZO)
Hussein Makame-MAELEZO
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith
Mahende ametoa miezi minne kwa kiwanda cha M.M Integrated Steel Mills Ltd kiwe
kimefunga mitambo ya kutibu majitaka yanayozalishwa na kiwanda chao.
Waziri Dkt. Mahenge alitangaza hatua hiyo wakati
akiwa kwenye ukaguzi kwenye kiwada hicho kilichopo jijini Dar es Salaam, ikiwa
ni mfululizo wa ukaguzi anaoendelea kuufanya kwenye viwanda mbalimbali jijini
humo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Baraza la Taifa la
Hifadhi ya Mazingira (NEMC) iliyo chini ya ofisi hiyo, kupokea malalamiko
kutoka kwa wanafunzi wa Chuo cha Kodi kilicho jirani na kiwanda hicho kuwa
wanaathirika na majitaka ya kiwanda hicho.
Mbali na kupewa sharti la kufunga mitambo hiyo,
Waziri Dkt. Mahenge aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuwasilisha Mpango wa Kuhifadhi
Mazingira wa kiwanda hicho baada ya miezi mitatu ambao kuwepo kwake kunatiliwa
shaka.
Hatua hiyo ilitokana na kiwanda hicho kushindwa
kumridhisha waziri juu ya wapi wanaupeleka
mchanganyiko wa mabaki ya madini mbalimbali yanayotumiwa na kiwanda
hicho baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa hutumika kinyume na taratibu.
Mbali na hayo, Waziri Dkt. Mahenge alitoa miezi
mitatu wawasilishe ripoti ya ukaguzi wa mazingira kinyume cha hapo watatozwa
faini na NEMC kwa mujibu wa sheria kwani hawaruhusiwi kuendesha kiwanda katika
hali hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa kiwanda hicho
Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda hicho, Lawrence Manyama alisema watatekeleza
maagizo hayo ingawa alidai kwa sasa wameacha kugawa mchanganyiko wa madini
kwenye viwanda.
Katika kiwanda cha BIDCO Oil & Soap Ltd, Waziri
huyo alitoa muda wa miezi 6 kwa kiwanda hicho kuacha kutumia magogo ya miti
kama vyanzo vya nishati kwani matumizi hayo yanachangia kuharibu mazingira.
Alisema gharama za kukabilaiana na mabadiliko ya
tabianchi yanayochangiwa na matumizi ya chanzo hicho ni kubwa sana kwa Serikali
lakini pia kwa karne ya sasa kiwanda hicho kinatakiwa kuacha kutumia chanzo
hicho.
Hata hivyo, mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho
Elias Nchwari aliponea chupuchupu kuwekwa ndani ya Mwanasheria wa NEMC Manchare
Heche,baada ya kumjibu vibaya Waziri Dkt. Mahenge wakati aliwasili kwenye
kiwanda hicho.
Katika hatua
nyingine Waziri Dkt. Mahenge alikipongeza kiwanda cha Cocacola Kwanza kwa
kupiga hatua kubwa ya mabadiliko ya matumizi ya nishati na katika kuhifadhi
mazingira kwa kutumia mitambo ya kisasa kutibu majitaka.
Hata hivyo, aliutaka uongozi wa kiwanda hicho uwe
mabalozi kwa viwanda vingine ambavyo havizingatii kuhifadhi mazingira katika
uzalishaji wao, hivyo kuwa chanzo kikubwa cha kuchafua mazingira.
Naye Meneja Mkazi wa Uzalishaji wa kiwanda hicho
Luois Coetzee alisema pamoja na gharamu kubwa waliyotumia katika nishati na
mitambo ya kutakatisha majitaka, lengo lao kubwa na kuhakikisha wanafanya mambo
kwa usahihi wake.
Mtaalamu wa Mitambo ya Kutakatisha Majitaka Emiliana
Kweka alisema wanalazimika kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa maji
yanayotoka kwenye kiwanda hicho yanakuwa salama kwa mazingira na viumbehai.
No comments:
Post a Comment