SHIRIKISHO
la Michezo ya Wizara na Idara za Serikari (SHIMIWI) limeanza kufanya usajili wa
wachezaji watakaoshiriki Michezo ya watumishi wa Serikali (SHIMIWI) itakayofanyika Mjini Dodoma kuanzia tarehe 27 Septemba hadi 11 Oktoba, 2014.
Watumishi
hao watashiriki katika Michezo ifuatayo;
1. Mpira
wa Miguu (Wanaume)
2. Netboli
(Wanawake)
3. Kuvuta
Kamba (Wanaume na Wanawake)
4. Riadha
(Wanaume na Wanawake)
5. Baiskeli
(Wanaume na Wanawake)
6. Karata
(Wanaume na Wanawake)
7. Bao
(Wanaume na Wanawake)
8. Drafti
(Wanaume na Wanawake)
9. Darts
(Wanaume)
Usajili
huo umeanza rasmi tarehe 27 juni, 2014 na unatakiwa kukamilika ifikapo tarehe 31 Agosti,2014. Shirikisho linaomba
kila Kadi ya usajili wa Mchezaji iambatane
na vifuatavyo;
1. Kitambulisho cha kazi
2. “Salary slip” ya karibuni
3. Kitambulisho cha Bima ya Afya
Aidha,
Klabu zitakazoshiriki zinatakiwa kuthibitisha kwa kutaja aina ya Michezo
watakayocheza kabla ya tarehe iliyotajwa hapo juu.
Moshi Makuka
KAIMU KATIBU MKUU (SHIMIWI)
Imetolewa leo
tarehe 10 Julai, 2014.
No comments:
Post a Comment