Naibu waziri mkuu nchini
Uingereza Nick Clegg ametoa wito wa Urusi kupokonywa haki za kuandaa
mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2018.
Ameliambia gazeti la Sunday Times kwamba
haiwezekani kwa michuano hiyo kufanyika nchini humo kufuatia hatua ya
Urusi kuwaunga mkono waasi wa Ukraine mashariki mwa taifa hilo
wanaoushukiwa kwa kuitungua ndege ya abiria ya Malaysia hivi majuzi.Amesema kuwa ulimwengu utaonekana myonge iwapo utaruhusu michuano hiyo kuendelea nchini Urusi.
Urusi imelaumu Ukraine kwa kuanguka kwa ndege hiyo iliowauawa takriban watu 300.
No comments:
Post a Comment