TANGAZO


Sunday, July 27, 2014

Mwandishi Heny Lyimo afariki dunia kwa ajali ya pikipiki


Baadhi ya waandishi wa habari, watangazaji na waombolezaji, wakiwa katika msiba huo, nyumbani kwa mama yake mkubwa, marehemu Heny Lyimo leo.  (Picha zote na Paul Wilium)
Baadhi ya waandishi wa habari, watangazaji na waombolezaji, wakiwa katika msiba huo, nyumbani kwa mama yake mkubwa, marehemu Heny Lyimo leo.
Marehemu Henry Lyimo akiwa katika studio za Moshi fm enzi za uhai wake.
 Marehemu Heny Lyimo

Na Paul Wilium, MOSHI.
WADAU wa Habari na Michezo mkoani Kilimanjaro, wamegubikwa na siminzi na vilio, baada ya Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa kituo cha Moshi Fm radio, kufariki dunia.

Mwandishi huyo, Henry Lyimo alimaarufu Kipesa mchezaji nguli na ghali kuliko wote barani Afrika, alifariki dunia baada ya usafiri aliokuwa akiutumia wa pikipiki kugongana na piki piki nyingine katika makutano ya barabara ya Marangu- Rombo, katika kijiji cha Himo, wilayani Moshi mkoani hapa.

Akizungumzia kifo hicho, Katibu wa Chama cha waandishi wa Habari (MECKI), mkoani hapa Nakajumo James, alisema taarifa za kifo cha mwandishi huyo, wa Habari na Mtangazaji, alizipata Julai 26, mwaka huu majira ya saa mbili za usiku.

James alisema baada ya kupata taarifa hizo kwa wasamaria wema, alituma mwindishi wa habari na mtangazaji mwenyake wa kituo hicho, ili kwenda katika eneo la tukio kuthibitisha taarifa hizo.

Alisema baada ya mfanyakazi mwenzake kufika katika eneo la tukio alikuta mwili wa marehemu umeshaondolewa na Jeshi la polisi na kwenda kuhifadhiwa katika hospitali ya Kilema, ambapo alifwatilia katika hospitali na kukuta taarifa hizo ni za kweli.

“Baada ya kupata taarifa za mwandishi mwenzetu wa Habari kufariki dunia, nilipatwa na mshtuko mkubwa na kuona kama taarifa hizo si za kweli, ambapo nilianza kuwasiliana na viongozi wenzangu na kuamua kumtuma mmoja wa viongozi kwenda katika eneo la tukio ili kuhakikisha kuwa taarifa hizo ni za kweli” alisema Jemsi.

WAANDISHI WA HABARI WALICHUKULIAJE TUKIO HILI.

Waandishi wa Habari mkoani Kilimanjaro, wamelipokea tukio hili kwa siminzi kubwa kutokana na ushirikiano mzuri wa kujitolea wa marehemu huyo ambapo kila mmoja alionyesha nyuso za siminzi na uzuni mkubwa.

Mmoja wa waandishi wa Habari na Mtangazaji wa Moshi fm radio, Bahati Mustafa Nyakiraria, alisema siku ya tukio hilo, majira ya jioni aliwasiliana na Marehemu huyo akimsihi kuwahi mapema ili waongoze kipindi cha michezo, katika radio hiyo kinachoanza majira ya saa mbili na nusu za usiku.

“Jana usiku majira ya jioni, niliwasiliana na Kipesa na kumweleza kuwa tutakuwa nae katika kipindi cha Michezo majira ya saa mbili na nusu za usiku na kumsihi awahi, baada ya hapo sikuwasiliana nae paka napokea taarifa za umauti wake” alisema Mustafa.

Marehemu huyo ambaye pia alikuwa ni mdau mkubwa sana wa michezo mkoani Kilimanjaro anategemewa kuzikwa leo (kesho), baada ya ndugu wa marehemu kuwasili nyumbani.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Robert Boaz, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa baada ya pikipiki hizo mbili kugongana dereva wa piki piki nyingine alikimbia kusikojulikana na jeshi la polisi linaendelea na msako ili kumkamata.

Kamanda Boaz, ametoa pole kwa Familia, Waandishi wote wa Habari mkoani hapa na Taifa pamoja na wadau wa michezo kwa ujumla kwa kupotelewa kwa mpiganaji nguli kama Henry Lyimo.

Mungu ametoa na Mungu ametwaa jina la Bwana  lihimidiwe, kwa niaba ya kampuni ya Jambo Concepts, tunapenda kuwapa pole wafiwa wote na wadau wa habari na Michezo kote nchini, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kizito.

No comments:

Post a Comment