Mwenyekiti
wa Kikundi cha Waendesha pikipiki Likotwa, Manispaa ya Lindi, Bw. Maulid Said
Mohamed (kushoto), akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw.
James Kajugusi risala kuhusu kikundi
hicho hivi karibuni Mjini Lindi. Mkurugenzi huyo alitembelea
kikundi hicho ili kukagua jinsi kikundi hicho kinavyofanya kazi na jinsi
kinavyonufaika na umoja huo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Lindi, Bw.
Daniel Kanuse. (Picha
na Concilia Niyibitanga)
Na Concilia Niyibitanga - Ofisa Habari -WHVUM
SERIKALI
inatarajia kukopesha vikundi vya uzalishaji mali vya vijana vipatavyo 453
katika mwaka wa fedha 2014/15 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James
Kajugusi alipotembelea kikundi cha Vijana waendesha pikipiki cha Likotwa
kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Lengo
la Serikali ni kuhakikisha kuwa vijana wanajiajiri wenyewe na kuondokana na
dhana ya kutegemea kuajiriwa ikizingatiwa kuwa kila mwaka vijana wapatao
milioni 1.2 huhitimu vyuo vikuu lakini wanaopata ajira za kuajiriwa ni vijana
200 tu. Amesema Bw. Kajugusi.
Mikopo
inayotolewa kwa vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ni njia ya
kuwakomboa vijana kwa kuwaongezea mitaji ya kuweza kufanya shughuli za ujasiri
na ujasiriamali na hatimaye kujiajiri na kuajiri vijana wenzao.
Bw.
Kajugusi amekipongeza Kikundi cha Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda cha
Likotwa kwa juhudi na mafanikio waliofikia hadi sasa kutokana na kuunda kikundi
hicho chenye lengo la kuboresha maisha ya waendesha pikipiki hao.
Aidha,
amewataka kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuzingatia maadili mema ili
kuimarisha amani na mshikamao katika
sehemu wanazoishi na vile vile
kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kama vijana wa kulipa kodi.
Halikadhalika,
amekitaka kikundi hicho kuwahamasisha vijana wenzao kushiriki katika shughuli
za Mbio za Mwenge wa Uhuru na kuwaeleza manufaa ya mbio hizo na kuwapuuza
wanobeza Mwenge kwani wanaoubeza ni watumwa kwani wanaibeza historia ya nchi yao.
Naye
kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Bw. Maulid Said Mohamed amesema kuwa kikundi kina wanachama 13 na
pikipiki 2 zinazomilikiwa na kikundi na
hadi sasa wameshapatiwa viwanja 6 na Uongozi wa Manispaa kwa ajili ya kufanya
shughuli za maendeleo ya Kikundi.
Bw.
Mohamed amesema kuwa mpaka sasa kikundi kimejiwekea akiba na lengo kuu ni
kuanzisha SACCOS kwa ajili ya kuwakopesha vijana kwa riba nafuu na hatimaye
kutengeneza ajira kwa vijana wengi zaidi.
Kikundi
cha Waendesha pikipiki Likotwa kina wanachama 13 na kilianzishwa kwa nia ya
kusaidiana na kujiinua kiuchumi na kina malengo ya kuanzisha SACCOS kwa ajili
ya kukopesha vijana mikopo yenye masharti nafuu.
No comments:
Post a Comment