TANGAZO


Friday, July 11, 2014

Moto uliodumu kwa zaidi ya saa tatu wawatia umasikini zaidi ya watu 100 mkoani katika eneo la Jamatini, Dodoma

Baadhi ya watu wa mji wa Dodoma, wakisaidia kuzima moto uliokuwa ukiendelea kuteketeza mabanda ya wafanyabiashara katika soko la mitumba la Jamatini, maarufu kama Sarafina baada ya moto huo kuzuka, kuanzi kwenye banda la vinyago usiku wa kuamkia leo. (Picha zote na John Banda)
Wafanyabiashara katika eneo la Sarafina, Manispaa ya Dodoma wakisikitika walipokuwa wakiangalia moto uliokuwa ukiteketeza mabanda pamoja na mali zilizokuwa ndani, chanzo cha moto huo bada hakijajulikana.
Wakazi wa Dodoma Wakijaribu kuudhibiti moto mkubwa uliokuwa ukiteketeza mali na mabanda ya wafanyabiashara wa mitumba katika eneo la jamatini  kwa kutumia mchanga na matawi ya miti ili usiendelee baada ya kudumu zaidi ya saa tatu huku zaidi ya mabanda 80 yakiteketea.
Moto mkubwa ukiendelea kuteketeza mabanda ya wafanya biashara wa maduka na mitumba katika eneo la Sarafina Dodoma.
Moto ukiendelea kuteketeza mabanda ya wafanyabiashara wa maduka na mitumba katika eneo la Sarafina, mjini Dodoma.
Wafanyakazi wa Zimamoto wakiendelea kuwajibika wakati walipokuwa wakizima moto katika eneo la Jamatini linalopakana na baa ya Actik, ambapo zaidi ya vibanda 80 viliteketea zikiwemo mali za wafanyabiashara wa eneo hilo lililopo Manispaa ya Dodoma.
Bidhaa mbalimbali zikiwa zimezagaa baada ya kutolewa kwenye moja ya mabanda yaliyokuwa yakiungua kutokana na moto ambao bado haujajulikana chanzo chake katika eneo la nyuma ya kituocha Daladala Jamatini Dodoma.

No comments:

Post a Comment