Mtoto
Gloria Fusi mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la kwanza katika
shule ya msingi Utwango wilayani Namtumbo akiandika jina lake katika
Notebook ya Mama Salma Kikwete wakati Rais Kikwete aliposimama katika
kijiji cha Utwango kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea mjini
Namtumbo akitokea Songea mjini. Mtoto Gloria alimsalimia Mama Kikwete
kwa uchangamfu na ndipo Mama Salma alipomuuliza kama anajua kuandika
jina lake na hivyo kumpatia notebook yake na mtoto huyo bila kusita
aliandika vizuri jina lake.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia Mzee Mustafa Mangunyuka muda
mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa michezo wa Taifa wilayani
Namtumbo ambapo aliwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mbunge wa Namtumbo Mh. Vita
Kawawa muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kuwahutubia mamia ya wakazi wa
Namtumbo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa
mjini Namtumbo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia mamia ya wakazi wa Namtumbo katika Uwanja wa Taifa mjini Namtumbo leo.
Mamia
ya Wakazi wa Namtumbo waliohidhuria mkutano wa hadhara ulihutubiwa na
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo katika Uwanja wa Taifa mjini Namtumbo
(Picha zote na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment