Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu akishauriana na maafisa wake leo.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia
tukio la mlipuko wa bomu siku ya tarehe 7/7/2014 majira ya saa 22.15
usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha, ambapo
watu wanane walijeruhiwa, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 25 kwa
uchunguzi. Kufuatia uchunguzi huo kati yao watu sita watafikishwa
mahakamani mapema iwezakanavyo.
Watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo ni:
1. SHAABAN MUSSA MMASA @ JAMAL, Umri miaka 26 Kabila, Msambaa. Mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo.
2.
ATHUMAN HUSSEIN MMASA, Umri miaka 38 kabila Msambaa, Mlinzi katika
Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la GYMKHANA jirani na eneo la tukio.
3. MOHAMED NURU @ MUHAKA, Umri miaka 30 Kabila Msambaa, Mlinzi katika mgahawa wa Chinese jirani na eneo la tukio.
4.
JAFFAR HASHIM LEMA, Umri miaka 38 Mchaga Mwalimu wa Shule ya Msingi
Olturmet Wilaya ya Arumeru. Pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA mjini
Arusha. Huyu ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya
milipuko ya mabomu maeneo mbalimbali nchini.
5. ABDUL MOHAMED HUMUD SALIM,@Wagoba; umri wa miaka 31, Mmanyema wa Ujiji Kigoma, wakala wa Mabasi Stendi Arusha.
6. SAIDI MICHAEL TEMBA; umri wa miaka 42, Mchaga, mfanyabiashara wa Arusha.
Aidha
tarehe 21/07/2014 majira ya saa 20.00 usiku maeneo ya Sombetini
walikamatwa YUSUFU HUSSEIN ALLY @ HUTA, kabila Mrangi, umri wa miaka 30
na mkewe SUMAIYA JUMA , kabila mwasi umri wa miaka 19 wakiwa nyumbani
kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono saba,
risasi sita za shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa
kufika nusu kilo na bisibisi moja. Mtuhumiwa YUSUFU HUSSEIN ni miongini
mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote
jijini Arusha. Mahojiano yanaendelea dhidi yake.
Uchunguzi
wa shauri hili pamoja na matukio mengine ya milipuko unaendelea, ikiwa
ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa Polisi na
kuwakamata watakao bainika kuhusika na matukio hayo, mtajulishwa matokeo
ya uchunguzi huo mara utakapokamilika.
Hata
hivyo Jeshi la Polisi linatangaza kumtafuta YAHAYA HASSAN HELLA, kabila
mrangi, umri wa miaka 33, mkazi wa Mianzini Arusha, mwenye asili ya eneo
la Chemchemu Kondoa Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya
ulipuaji mabomu nchini. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye toa
taarifa zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu huyu.
Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa. Asanteni.
………………...…………..
ISAYA MNGULU-CP
MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA
No comments:
Post a Comment