Na Winner Abraham
14/07/2014
KAMPUNI ya utengenezaji magodoro ya Vita Foam imepokea cheti cha uthibitisho ya ISO 9001:2008 na bar code ya kutokana na kutimiza viwango vya usimamizi wa kutimiza wa ubora kinachotambulika kimataifa.
Hayo yamesemwa leo, jijini Dar-es-Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Suraj Chandalia wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).
Ameongeza kwa kusema kuwa kampuni yao inakuwa ya kwanza na ya kipekee ya kutengeneza magodoro Tanzania kufikia uthibitisho ISO 9001:2008.
“Cheti hicho kimefanyiwa utathimini na kupitishwa na bodi maalum ya uthibitisho linalojulikana kimataifa, QAS international na ndicho cheti kinachopanga vigezo kwa ajili ya mfumo wa usimamizi bora na kinatoa mfumo muhimu ya kuboresha ufanisi wa kampuni, kupunguza hali ya hatari na kuongeza nafasi,” alisema Chandalia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko Tanzania kutoka kampuni ya GS1, ambayo ndiyo imetoa cheti hicho, Ester Budili ameishukuru kampuni ya Vita Foam kwa kuwashirikiana na kampuni yao, kwani wameonyesha uzalendo wa hali ya juu na kuyataka makampuni mengine kutosita kushirikiana nao. Ambapo walimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa Vita Foam Suraj Chandalia cheti cha bar code ya bidhaa.
Vita Foam ikiwa kampuni iliyosajiliwa mwaka 1999 ni watengenezaji pekee Tanzania kwa kuzalisha magodoro ya spring ndani ya nchi zikiwemo zilizotengenezwa kwa aina mbalimbali ya spring ya mfukoni na bonnel au isiyo na mifuko.
Vita Foam imefanikiwa kuwa na mitambo yake sehemu mbalimbali nchi kama Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha na Tanga. Ambapo pia hutumika majumbani, kati ka mahoteli, mahospitali, mashuleni na hata vyuo vikuu.
No comments:
Post a Comment