TANGAZO


Monday, July 21, 2014

FIFA yaondoa marufuku ya Nigeria


Rais wa FIFA Sepp Blatter

Shirikisho la soka duniani FIFA limendoa marufuku lililoiwekea Nigeria.
Shirikisho hilo lilikuwa limeipiga marufuku Nigeria kutoshiriki katika michuano yoyote ya soka mapema mwezi huu kwa kuwa serikali ya Nigeria iliingilia uongozi wa shirikisho hilo nchini Nigeria.
Hatua hiyo ya kuondoa marufuku hiyo inajiri baada ya mahakama kuondoa agizo la kuwatoa baadhi ya maafisa wakuu wa shirikisho hilo nchini Nigeria.
Kwa miongo kadhaa serikali za afrika zimekuwa na ushawishi wa mashirikisho ya soka katika mataifa yao hadi FIFA ilipoondoa uwezo huo.

No comments:

Post a Comment