TANGAZO


Tuesday, July 15, 2014

Benki ya KCB yajikita zaidi kusaidia jamii


*Yakabidhi misaada ya vifaa vya Hospitali  vyenye thamani ya shilingi milioni 15, mkoani Kilimanjaro 
Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa, Mawenzi, Dkt. Lwezaula Fredrick(katikati) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa misaada ya vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka kwa benki ya KCB Tanzania mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro. Wakisikiliza kwa makini ni meneja wa tawi la Moshi benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo(kushoto), Kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo(wapili kulia), ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo na katibu tawala msaidizi, afya na ustawi wa jamii, Dkt. Mtumwa Mwako.
Meneja wa tawi la Moshi benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi misaada ya vifaa vya hospitali yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi-Moshi mjini. Kushoto kwake ni Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa, Mawenzi, Dkt. Lwezaula Fredrick, Kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo na katibu tawala msaidizi, afya na ustawi wa jamii, Dkt. Mtumwa Mwako.
Kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo(kulia) akitoa shukurani zake kwa niaba ya mkoa baada ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka kwa benki ya KCB Tanzania kwa hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi mjini Moshi. Pamoja naye ni meneja wa tawi la Moshi benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo(kushoto) na mganga mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi, Dkt. Lwezaula Fredrick.
Meneja wa tawi la Moshi, benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo(wapili kushoto) akishikana mikono na kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo(kushoto) kama ishara ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni 15 katika hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi mjini Moshi. Wakifurahia tukio hilo ni mganga mfawidhi hospitali ya Mawenzi, Dkt. Lwezaula Fredrick(kulia) na katibu tawala msaidizi, afya na ustawi wa jamii, Dkt. Mtumwa Mwako.


Mteknolojia mionzi, Gerald Shuware(kushoto) akimuonesha kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo (kulia) namna mashine ya 'Ultra Sound' inavyofanya kazi baada ya benki ya KCB Tanzania kukabidhi msaada huo na vifaa vingine vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi mjini Moshi. Katikati ni meneja tawi la Moshi, benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo.
Mkazi wa kata ya Rau, Michael Mauki akizungumza na waandishi wa habari juu ya changamoto walizokuwa wakizikabili kabla ya kuwa na mashine ya Ultra Sound katika hospitali ya Mawenzi mjini Moshi. Mauki alisema wakazi wa Moshi mjini walilazimika kwenda hospitali za mbali kwa ajili yakufwata kipimo hicho cha Ultra Sound.
Baadhi ya madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi, wafanyakazi wa KCB Tanzania mjini moshi na wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro, moshi mjini wakifwatilia kwa makini hafla ya kukabidhiwa kwa misaada ya vifaa vya hosoitali kutoka kwa bsnki ya KCB Tanzania kwa hispitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi Moshi mjini.


WAKAZI wa Mkoa wa Kilimanjaro, hususani wakina mama wajawazito na wananchi wa mkoa huo, wameondokana na adha ambayo walikuwa wakiipata wakati walipokuwa wakifika katika hospitali ya Rufaa ya mkoa  Mawenzi, kwa ajili ya matibabu baada ya hospitali hiyo kupatiwa msaada wa mashine ya Ultra sound kutoka benki ya KCB Tanzania.

Mkazi wa kata ya Rau, Michael Mauki ambaye alishawahi kupati adha hiyo hospitalini hapo, alisema wagonjwa wengi ambao walikuwa wakifika katika hospitali hiyo walishindwa kufanyiwa uchunguzi kutokana na kutokuepo na mashine hiyo.
Mauki aliwahi kufika katika hospitali hiyo kwa lengo la kupima
ugonjwa wa  Figo, lakini alishindwa kuhudumiwa kutokana na kutokuwepo kwa kipimo hicho, na kusema kwamba kuwepo kwa mashine hiyo itasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wengi wakiwemo wa mama wajawazito.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo ya mkoa, Mawenzi, Dkt. Lwezaula Fredrick, alisema kwa takribani mwaka mmoja na nusu hospitali hiyo ilikuwa haina kifaa hicho hivyo wagonjwa walikuwa wakilazimika kwenda katika hospitali za binafsi na ya rufaa ya KCMC kwa ajili ya kufuata vipimo.
 
"Mama wajawazito ambao walikuwa wakifika hapa kwa ajili ya kupima walikuwa wakipata changamoto kubwa ya ukosefu wa kifaa hicho, tunaishukuru benki ya KCB Tanzania kwa kutoa msaada huu wenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa lengo la kutatua adha waliyokuwa wakiipata wagonjwa hao," alisema Dkt. Fredrick.

Dkt. Fredrick alisema wagonjwa wengi walikuwa wakilazimika kwenda katika hospitali binafsi na kutibiwa kwa gharama kubwa, na kwamba kuwepo kwa mashine hiyo katika hospitali hii itatatua changamoto hiyo.

Awali akikabidhi mashine hiyo ya ultra sound meneja wa benki hiyo  tawi la Moshi mjini, Oforo Erasmo, aliwaomba kuitumia mashine hiyo vizuri na kuitunza ili idumu pamoja na kuwasaidia wagonjwa wengi wa mkoa huo.

Erasmo alisema kwa mwaka huu KCB imetenga jumla ya shilingi Milioni 350 kwa ajili ya kusaidia jamii inayowazunguka na wateja wake kwa ujumla  katika nyanja za kielimu, afya, maji na mazingira.

No comments:

Post a Comment