TANGAZO


Thursday, July 17, 2014

£8m zamhamisha Demba Ba hadi Uturuki





Demba Ba sasa kuvaa jesi ya Besiktas ya Uturuki

Usajili mpya na mikataba mipya kwa wachezaji vinara ndio shughuli kuu inayoendelea sasa kabla msimu mpya wa michuano kuanza..
Pamoja na kasheshe zinazomuandama, Suarez sasa yuko Bacelona 100% baada ya kuihama Liverpool, nae Demba Ba tayari amewasili Uturuki anakotarajiwa kukamilisha uhamiaji wake kutoka Chelsea hadi Besiktas kwa gharama ya £8m.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa mika 29 ameyathibitisha hayo katika mtandao wa Twitter akionekana tayari kavalia jesi ya Besi-ktas. "Amesema yaliyobaki ni kukamilisha ukaguzi wa kiafya na kuweka saini mkatba.
Demba Ba amewahi kuifungia Chelsea angalau mabao 14.
Hivyo Chelsea wamejibu kwa kumshawishi Filipe Luis aihame Atletico Madrid ingaje Mbrazil huyo yuko katika safu ya ulinzi.
Msimu uliopita Luis alishiriki mechi zaidi ya 40 na kilele ikawa Atletico kushinda la liga kwa mara ya kwanza tangu 1996 na pia wakafikia fainali ya Champions League.

No comments:

Post a Comment