TANGAZO


Thursday, June 12, 2014

Watanzania kunufaika na Semina Maalum ya uongozi bora

Mkurugenzi Mtendaji  wa Mikono Business Consult Deogratius Kilawe kushoto  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu semina maalum ya uongozi bora itakayofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kesho, siku ya Ijumaa tarehe 13 Juni. Anayemuangalia kulia ni msemaji katika semina hiyo Azim Jamal kutoka Canada.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Mikono Business Consult Deogratius Kilawe kushoto  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu semina maalum ya uongozi bora itakayofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kesho, siku ya Ijumaa tarehe 13 Juni. Wa pili kulia ni msemaji katika semina hiyo Azim Jamal kutoka Canada na kushoto ni Msemaji wa masuala ya uongozi na maendeleo kutoka Marekani, Brian Tracy.
Mkurugenzi wa Mikono Business Consult Themi Rwegasira akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu semina maalum ya uongozi bora itakayofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere  tarehe 13 Juni. Wa pili kushoto ni msemaji wa siku hiyo, Brian Tracy kutoka Marekani, Mkurugenzi Mtendaji wa Mikono Business Consult, Deogratius Kilawe (wa tatu) na Azim Jamal msemaji kutoka Canada.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, James Rhombo akiongea na waandishi wa habari namna ambavyo Shirika la Nyumba limeweza kuhamasika na kuwadhamini baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika kidato cha nne ili waweze kuhudhuria semina hiyo,kushoto kwake ni Msemaji wa masuala ya uongozi na maendeleo kutoka Canada Azim Jamal.
Msemaji wa masuala ya uongozi na maendeleo kutoka Canada Azim Jamal (kulia), akielezea umuhimu wa semina maalum ya masuala ya uongozi kwa vijana itakayofanyika kesho, tarehe 13 Juni, ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mikono Business Consult, Deogratius Kilawe na kushoto ni msemaji wa siku hiyo, Brian Tracy kutoka Marekani.
Msemaji wa masuala ya uongozi na maendeleo kutoka Marekani, Brian Tracy (katikati), akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Mikono Business Consult, Deogratius Kilawe na kushoto ni Mkurugenzi wa Mikono Business Consult, Themi Rwegasira.
Wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne kwa ufaulu wa daraja la kwanza nchini, amabao wamedhaminiwa na Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC), kuweza kuhudhuria semina maalumu ya uongozi bora, itakayotolewa na wasemaji maarufu kuhusu masuala ya uongozi na maendeleo, Bw. Brian Tracy kutoka Marekani na Azim Jamal kutoka Canada.
Wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne kwa ufaulu wa daraja la kwanza nchini, amabao wamedhaminiwa na Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC), kuweza kuhudhuria semina maalumu ya uongozi bora, itakayotolewa na wasemaji maarufu kuhusu masuala ya uongozi na maendeleo, Bw. Brian Tracy kutoka Marekani na Azim Jamal kutoka Canada.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa leo jijini Dar es Salaam, kuhusu semina maalum ya uongozi itayofanyika kesho, tarehe 13 Juni ukumbi wa Mwalimu Nyerere. (Picha na Lorietha Laurence –Maelezo)

Na Lorietha Laurence-Maelezo
WASEMAJI mashuhuri  katika masuala ya uongozi bora na maendeleo Bw. Brian Tracy kutoka Marekani na Azim Jamal kutoka Canada wataongoza semina maalum ya uongozi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kesho, Juni 13 kwa vijana wa Kitanzania.

Wakiongea na waandishi wa habari leo jijini dare s Salaam wataalum hao wemesema ni muhimu kuwepo kwa semina hiyo ambayo itawasaidia vijana katikati uongozi na hivyo kuwa na fursa nzuri ya kuajiriwa katika ngazi za juu badala ya kuwapa wageni nafasi hizo,

“Ni vizuri kuhudhuria semina hii kwasababu kupitia semina hii ina mafunzo mazuri kuhusu uongozi  bora kwa kupata mbinu muhimu za uongozi bora kuanzia ngazi ya kampuni hadi ya Taifa hivyo” alisema Brian

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mikono Business Consult aliongeza kwa kusema semina hii itasaidia kuleta maendeleo katika nchi yetu hususani katika nyanja ya uongozi kwa kuweza v kuwa  na viongozi bora wa baadaye watakaofuata taratibu,kanuni na sheria za uongozi katika sehemu zao za kazi.

“kama ukiangalia katika Makampuni makubwa  na Taasisi  za kifedha utaona kuwa ni watanzania wazawa wachache tu ndio wako katika ngazi za juu za uongozi ambapo asilimia 96 ni wageni na asilimia 4 ndio wazawa  kupitia semina hii itabadilisha  utaratibu kwa kuwa na asilimia kubwa ya wazawa katika uongozi wa juu.” Alisema  Deogratius

Semina hii inawalenga watu wote kutoka katika sekta binafsi, sekta za umma,taasisi za kijamii,makampuni ya umma,viongozi wa Kiserikali pamoja  na wale wote waliokatika uongozi  ili kuweza kujijenga zaidi katika enao la uongozi na kupata matokeo mazuri yenye kuleta maendeleo kwa jamii yetu ya Tanzania.

Vilevili Bw. Brian Tracy ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kimataifa ya Brian Tracy ambayo inajishughulisha na kutoa mafunzo ya maendelao kwa watu mbalimbali,vilevile ameweza kusaidia makampuni 1000,na kuongea na watu milioni tano katika nchi arobaini duniani,pia ameweza kuandika vitabu 45 katika lugha mbalimbali.

Naye Azim Jamal ni mwanzilishi na mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc kampuni inayojishughulisha na kusaidia wadau  na makampuni kupata stahiki katika kazi zao na ni mwandishi wa vitabu mbalimbali vilivyotafsiriwa katika lugha 10.


No comments:

Post a Comment