TANGAZO


Thursday, June 12, 2014

Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar, mwenyeji wa Mkutano wa Kutathmini utekelezaji wa usajili wa Chakula na Dawa kwa nchi za EA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohd Saleh Jidawi akifungua Mkutano wa siku mbili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kufanya tathmini ya utekelezaji wa usajili wa Chakula na Dawa kwa Mamlaka za udhibiti wa bidhaa hizo kwa Nchi wanachama.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohd Saleh Jidawi (wakatikati) waliokaa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa tathmini ya utekelezaji wa usajili wa Chakula na Dawa uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar.
Mratibu wa Mradi wa Usajili wa Chakula na Dawa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. John Patrick (aliesimama) akitoa maelezo kuhusiana na Mradi huo katika Mkutano uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar.
Ofisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Bi. Hidaya Juma Hamad akielezea changamoto wanazokabiliana nazo katika utekelezaji wa kazi za Bodi hiyo, (kusho) ni Meneja Operesheni wa Mradi wa Usajili wa chakula na Dawa wa nchi za Afrika Mashariki Apolo Muhaiwira.
Mrajis Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhani Othman Simai akijibu  masuali aliyoulizwa na wajumbe wa Mkutano huo, (kushoto) Mwenyekiti wa Mkutano Dkt. Jamala Adam Taib. (Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar)

No comments:

Post a Comment