Mgeni rasmi Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji wa Uchumi Dkt. Mary Nagu akifungua
semina ya Wabunge kuhusu Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki jana katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma. Kulia ni Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akisisitiza umuhimu wa Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Wabunge katika semina iliyofanyika jana ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Masuala ya Utafiti wa Uchumi na Sera Benki
Kuu ya Tanzania Dkt. Joseph Masawe akitoa mada juu ya Majukumu ya Benki Kuu ya
Afrika Mashariki na Benki Kuu Wanachama na
Nchi wanachama walivyojifunza kutoka Umoja wa Ulaya wakati wa semina ya Wabunge
iliyofanyika jana katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma.
Mchungaji Luckson Mwanjale,
mbunge wa Mbeya Vijjini akichangia hoja juu ya Itifaki ya Umoja wa Fedha wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki jana mjini Dodoma.
Sara Msafiri (Viti
Maalum) akichangia mada juu ya itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki wakati wa semina ya Wabunge iliyofanyika jana katika ukumbi wa Bunge
wa Msekwa mjini Dodoma. (Na Mpiga picha wetu)
No comments:
Post a Comment