Mmoja wa waanzilishi wa mfuko wa kuwasaidia waathirika wa moto soko la Mchikichini ambaye pia ni Meneja wa Vituo vya mizigo vya nchi kavu wa Kampuni ya AZAM Bw. Raymond Adolph akieleza namna walivyoguswa na tukio la moto lililotokea katika soko hilo na kuwaomba watanzania kuunga mkono juhudi hizo.
Mmoja wa waanzilishi wa mfuko wa kuwasaidia waathirika wa moto soko la Mchikichini ambaye pia ni Meneja wa Vituo vya mizigo vya nchi kavu wa Kampuni ya AZAM Bw. Raymond Adolph akieleza namna walivyoguswa na tukio la moto lililotokea katika soko hilo na kuwaomba watanzania kuunga mkono juhudi hizo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Mchikichini Bw. Jumanne Kongolo akiongea na waandishi wa habari kuishukuru serikali na wananchi waliojitokeza kufungua mfuko wa kuwasaidia waathirika wa moto katika soko hilo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mchikichini walioathiriwa na janga la moto wakifuatilia masuala mbalimbali ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kuwasaidia wafanyabiashara hao. (Picha zote na Aron Msigwa –MAELEZO)
Na
Aron Msigwa – MAELEZO.
20/6/2014.
Dar es Salaam.
Baadhi ya wakazi wa
jiji la Dar es salaam wamejitokeza kuanzisha mfuko maaluum wa kuwasaidia
wafanyabiashara wapatao 5700 wa soko la
Mchikichini walioathiriwa na janga la moto lililotokea usiku wa kuamkia tarehe 12 mwezi huu eneo la Karume,jijini Dar es salaam.
Akaunti hiyo maalum
inayojulikana kwa jina la Mkono wa Pole Chinga 2014 imefunguliwa katika Benki
ya CRDB Tawi la Lumumba ili kuwawezesha wadau mbalimbali wanaoguswa na tukio
hilo kutoa mkono wa pole kupitia akaunti namba 0152270491300.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia
ni mkuu wa wilaya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam amesema kuwa mfuko huo unalenga kurejesha hali ya maisha
waliyokuwa nayo wafanyabiashara hao hapo awali kabla ya kuungua kwa vibanda na
bidhaa zao.
Amesema akaunti hiyo
itasimamiwa kwa pamoja na wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam, wadau waanzilishi na wafanyabishara walioathirika.
“Tumeanzisha akaunti
hii kutokana na wananchi kuguswa na tukio hili kwa kuonesha nia thabiti ya
kutaka kutoa mkono wa pole kwa waathirika wa janga hili, nachoweza kusema jambo
hili tumeliwekea utaratibu na tutaliendesha kwa uwazi mkubwa kwa kushirikiana
na wahusika wa tukio” amesema Bw. Raymond.
Aidha, amefafanua kuwa
serikali kupitia Manispaa ya Ilala ambayo soko hilo liko chini yake
itahakikisha inaboresha hali ya miundombinu katika soko hilo zikiwemo barabara
za kuwezesha magari na vifaa vya uokoaji kupita wakati wa majanga ya moto huku
akiwataka wafanyabiashara hao kutojenga
na kuzuia maeneo ya barabara katika soko hilo.
Mmoja wa waanzilishi wa mfuko huo ambaye pia
ni Meneja wa Vituo vya mizigo vya nchi kavu vya vya Kampuni ya AZAM Raymond
Adolph ameeleza kuwa yeye kama mfanyakazi na wafanyakazi wengine wameguswa na
tukio la moto lililotokea katika soko hilo na kufafanua kuwa kiasi cha fedha
kitakachopatikana kitakabidhiwa kwa walengwa kwa uwazi huku akiwaomba
watanzania kuunga mkono juhudi hizo.
“Akaunti hii
tuliyoifungua itakuwa chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kiasi tutakachopata tutakikabidhi kwa
wahusika kwa uwazi na tunawaomba watanzania wajitokeze ili kwa pamoja tuwasaidie
ndugu zetu hawa waliopata matatizo” amesisitiza.
Kwa upande wake mwenyekiti
wa wafanyabiashara hao ambaye pia aliathiriwa na moto huo Bw. Jumanne Kongolo
ameeleza ameishukuru serikali na wananchi waliojitokeza kufungua mfuko huo kwa
lengo la kuwasaidia wafanyabiashara walioathirika na moto huo.
No comments:
Post a Comment