Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akifafanua
jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) wakati wa semina kwa
wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura
nchini, kulia ni Mkurugenzi wa uchaguzi toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.
Julius Mallaba.
Baadhi ya wahariri wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.
Baadhi ya wahariri wakimsikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo
pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa
wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura
nchini.
Baaadhi ya wakuu wa Idara toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifanya kazi yao kwa
umakini wakati Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian
Lubuva (hayupo pichani) wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya
habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.
Waandishi wa habari wakifanya kazi yao kwa umakini
wakati Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva
(hayupo pichani) wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu
ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.
Baadhi ya wahariri wakimfuatilia mtoa mada kwa makini toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Julius Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.
Baadhi ya wahariri wakimsikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo
pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa
wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura
nchini. (Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO)
Na Frank Shija,
Maelezo
19/06/2014
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) inatarijia kuanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura mapema mwezi Septemba 2014, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi
Mkuu wa Mwaka 2015 na upikaji wa Kura za Maoni kwa ajili ya mchakato wa Katiba
Mpy.
Hayo yamebainishwa na
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Damian Lubuva wakati
akifungua Mkutano wa NEC na Wahariri wa Vyombo vya Habari, jana jijini Dar es
Salaam.
Jaji Lubuva amebainisha
kuwa uborehasji wa Daftari la Wapiga kura litatumia mfumo mpya wa Kiteknolojia
ujulikanao kama Biometric Voter Registration (BVR) ambapo katika mfumo huo
taarifa za mtu za Kibiolojia au tabia ya mwanadamu zitachukuliwa na kuifadhiwa
kwenye kanzi data ya Wapiga Kura.
Katika mfumo huo
wananchi wote wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na Kadi za Mpiga
Kura watatakiwa kuandikishwa upya ili kupata Daftari sahihi linaloaminika zaidi
kwa ajili ya upigaji Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Uamuzi wa kutumia mfumo
huo mpya wa kuandikisha wapiga kura umefikiwa baada ya kubaini kasoro
mbalimbali zilizokuwepo kutokana nma kutumia mfumo wa zamani wa Optical Mark
Recognition (OMR) hadi kupelekea baadhi ya wadau wa uchaguzi kupigia kelele
mfumo huo.
Aliongeza kuwa
kutumiika kwa mfumo wa BRV kutasaidi kuondoa kabisa matatizo yaliyomo kwenye
Daftari lililopo ikiwemo kuzuia mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja.
“Ndugu zangu wahariri
ni ukweli ulio dhahiri kwamba matumizi ya OMR yalisababisha kwa kiasi kikubwa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuwa na kasoro,zilizopelekea baadhi ya wadau
wa uchaguzi kuhoji uhalali wake. Hivyo ni mategemeo ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kuwa matumizi ya BVR yatapunguza au kuondoa kabisa matatizo yaliyomo
kwenye Daftari lililopo”. Alisema Jaji Lubuva.
Aidha Jaji Lubuva
alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kutoa
ushirikiano kwa NEC ilikufanikisha zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga
Kura kwa kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi ili waapate uekewa wa
mfumo huu mpya utakaomtumika katika zoezi hilo, na kutoa hamasa wajitokeze
katika viotuo vya kujiandikishia.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Malaba amesema kuwa maandalizi ya zoezi la
uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura umekamilika kwa asilimia kubwa ikiwa ni
pamoja na kufanya uhakiki wa vituo vya kujiandikishia ambapo jumla ya vituo
40,015 vimeainishwa kutoka vituo 24,919 vilivyokuwepo awali.
Malaba aliongeza kuwa
ongezeko hilo la vituo limetokana na kushusha zoezi la uandikishaji wa Wapiga
Kura kutoka ngazi ya Kata, na sasa utafanyika kuanzia ngazi ya Vitongoj,Vijijii
na Mitaa ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wananchi.
Malaba aliongeza kuwa
Tume inatarijia kupokea vifaa kwa ajili ya zoezi hilo mapema mwezi Aguosti 2014
kwa aijili ya kuanza rasmi zoezi la
Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura, na kuongeza kuwa vifaa vichache vitawasili
mapema mwezi julai kufanikisha mafunzo kwa watendaji watakao husika na zoezi la
Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura.
Uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Mpiga Kura linatarijiwa kuanza mwezi septemba 2014 ambapo kila
kituo cha kujiandikisha kinakadiriwa kutumia siku 14 hadi zoezi kukamilika , na
jumla ya takribani shilingi Bilioni 293 zinatarajiwa kutumika katika zoezi
hilo.
No comments:
Post a Comment