Mkuu wa Wilaya ya Magharibi, Hassan Mussa Takrima akitoa nasaha kwa washiriki wa mafunzo ya siku tano juu ya mkakati wa Afya ya Jamii kwa viongozi wa Kamati za Afya za Shehiya, katika ukumbi wa Ofisi ya walemavu wa Kikwajuni Weiles, Mjini Zanzibar.
Ofisa Mipango na Utumishi wa Wilaya ya Magharibi Unguja, Bw. Ameir Ali Haji akitoa maelezo juu mafunzo ya siku tano kwa viongozi wa Kamati za Afya za Shehiya tatu za Magharibi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima ambae ni mgeni rasmin katika mafunzo hayo. Yaliofanyi ukumbi wa Ofisi ya walemavu Kikwajuni weles Mjini Zanzibar.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.
Muezeshaji kutoka Kitengo cha Elimu ya Afya ya jamii Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Amina Sleyum akitoa mafunzo juu ya Elimu ya Afya kwa jamii.
Washiriki wa semna hiyo, wakifanya mtihani.
(Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
MKUU wa Wilaya wa Magharibi, Hassan Mussa Takrima amewataka watendaji wa wizara ya afya kushirikiana na masheha katika kuelimisha wananchi juu ya utekelezaji wa mpango wa afya kwa jamii ili uweze kutatua changamoto za kifya nchini.
Amesema kuwa endapo mpango huo ukihamasishwa kwa jamii utaweza kuwasaidia wananchi katika kujikwamua na matatizo ya kujikinga na maradhi mbalimbali yanayojitokeza katika maeneo yao .
Akizungungumza katika ufunguzi wa mafunzo juu ya mkakati wa afya ya jamii kwa kamati kiongozi za shehia za Magogoni,Meli nne na Chukwani zilizopo katika wilaya Magharibi ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi katika kupunmguza matatizo ya kifya yanayozikabili shehia hizo.
Alieleza kuwa serikali ya mapinduzi Zanzibar imeamua kutoa fursa kwa watendaji wa sekta ya afya waweze kufanya kazi kwa mashirikiano na viongozi kuanzia ngazi ya shehia kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na afya bora.
“Tumieni mafunzo yenu vizuri kwa hekima na upole kwani nyinyi mnaenda kuielimisha jamii, na uko kuna makundi mbalimbali yanayotakiwa kupewa taaluma juu ya umuhimu wa kutunza afya na utekelezaji wa mpango huu kwa vitendo.”alisema Takrima.
Nae Afisa wa afya wa wilaya hiyo, Abubakar Mohamed Ali ameeleza kuwa katika katika mafunzo hayo washiriki watafundishwa njia mbadala ya kuwawezesha masheha na viongozi wengine kutumia rasilimali zilizomo katika maeneo yao ili kutatua changamoto za kiafya bila kusubili utekelezaji kutoka serikali kuu.
Kwa upande wake afisa mipango wa Wilaya hiyo Ameir Ali Haji alifamisha kuwa lengo la mkakati huo ni kuimarisha mahusiano baina ya sekta ya afya na jamii ili kuinua huduma za afya zinazotolewa ziweze kuendana na viwango vilivyowekwa na Serikali.
No comments:
Post a Comment