TANGAZO

Sunday, June 22, 2014

Ushiriki wa Mamlaka ya Usalama wa Anga katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar

Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege nchini Suleiman S. Suleiman (katikati), akiangalia mfano wa jengo la Tatu (Termina III), alipotembelea banda la Taasisi yake wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jana jijini Dar es Salaam. Jengo hilo linalojengwa katika eneo la Kipawa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) na linatarijiwa kutumiwa na Wasafiri wa Kigeni pindi litakapokamiilka.Mwenye kilemba kichwani ni Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bibi. Fatma Mtimba, anayemfuatia ni Meneja Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bw. Mohamed Ally na anayeelezea mfano wa Jengo hilo ni Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Bw. Geofrey Youze..

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchi Suleiman S. Suleiman (kushoto), akifurahia jambo alipokuwa akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, alipotembelea Maonesho ya Wiki wa Utumishi wa Umma leo, yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA Bw. Laurent Mwigune, Afisa Habari Mwandamizi Bi. Frida Nkondokaya na Afisa Sheria na Mahusiano Bi. Nuru Nyoni.

Ofisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Bw. Ally Z. Changwila akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi yao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Ofisa Vibali wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bw. Christopher Peter Sabuni (katikati), akielezea program yaKusaidi Wanafunzi wanaosomea masomo ya Urubani inayotolewa na Taasisi hiyo, kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka hiyo Bw. Ally Z. Changwila. TCAA mpaka sasa imekwisha saidi jumla ya wanafunzi watano walioenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya masomo ya Urubani na Uinjinia wa Ndege.

Ofisa Vibali wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bw. Christopher Peter Sabuni (katikati), akielezea program yaKusaidi Wanafunzi wanaosomea masomo ya Urubani inayotolewa na Taasisi hiyo, kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka hiyo Bw. Ally Z. Changwila. TCAA mpaka sasa imekwisha saidi jumla ya wanafunzi watano walioenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya masomo ya Urubani na Uinjinia wa Ndege. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)

No comments:

Post a Comment