Kampuni ya kawi nchini Urusi
Gazprom imesitisha usambazaji wake wa gesi kwa Ukraine baada ya siku ya
mwisho ya Ukraine kulipa deni lake la dola billioni mbili kukamilika.
Kamishna wa kawi katika muungano wa Ulaya
Guenter Oettinger amesema kuwa mataifa yanayotumia gesi katika muungano
huo hayafai kupata shida kwa kuwa Ukraine ina akiba kubwa ya gesi katika
hifadhi zake.Bwana Oettinger amesema kuwa mazungumzo yanayoshirikisha Urusi na Ukraine pamoja na mataifa mengine ya Ulaya kuhusu bei ya gesi ya Urusi yataendelea baadaye mwezi huu.
Kampuni ya Gazprom imesema kuwa ni muhimu kwamba mazungumzo hayo hayatasitishwa.
Muungano wa Ulaya unapata asilimia 15 ya gesi yake kutoka Urusi kupitia Ukraine.
Kampuni hiyo ya Urusi hata hivyo imesema kuwa itaendelea kuuza gesi yake barani Ulaya.
Uhusiano wa Urusi na Ukraine umezorota tangu Urusi iliponyakua eneo la Crimea mnamo mwezi February.
Ukraine imesema kuwa Urusi inaunga mkono wapiganaji wanaotaka kujitenga mashariki mwa taifa hilo.
No comments:
Post a Comment