Marekani inatathmini kuanzisha
mazungumzo ya moja kwa moja na Iran kuhusu mbinu za kukabiliana na
tishio kutoka kwa wanamgambo wa dhehebu la kisunni nchini Iraq
Ripoti zinasema kuwa huenda mazungumzo hayo yakang'oa nanga wiki hii.Mara kwa mara Marekani imekuwa ikiishtumu Iran kwa kuchochea ghasia nchini Iraq, lakini inaonekana kuwa mataifa hayo mawili yana nia ya kuzuia makundi ya kiislamu yaliyo na mipango ya kulidhibiti taifa hilo.
Wakati huohuo Marekani imelaani vikali picha za kuogofya zilizowekwa kwenye mtandao na watu wa Sunni ambazo zinaonyesha wapiganaji wakiwaua wanajeshi wa Iraq.
Jeshi la Iraq limeseama kuwa picha hizo zilikuwa za kweli lakini bado hazijathibitishwa.
Mwandishi wa BBC anasema ikiwa picha hizo ni za kweli, haya yatakuwa mauaji mabaya zaidi kufanywa dhidi ya wanajeshi wa Iraq tangu Marekani kuvamia Iraq mwaka 2003.
Picha hizo ziliibuka huku serikali ya Iraq ikisema imeweza kudhibiti waasi wa Kisuni na kutwaa maeneo waliyokuwa wameyateka nyara.
Wapiganaji wenye itikadi kali waliteka miji mikubwa ikiwemo Mosul na Tikrit, wiki jana, lakini miji kadhaa imedhibitiwa kutoka kwa waasi.
Hata hivyo wapiganaji hao wameteka mji wa Tal Afar, Magharibi mwa Mosul, usiku kucha baada ya mashambulizi makali.
No comments:
Post a Comment