TANGAZO


Friday, June 13, 2014

TIPER yakabidhi Serikali gawio la Shilingi 1,275,000





Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Servarcius Likwelile (wa pili kushoto), akipokea mfano wa hundi, yenye thamani ya sh. Bilioni moja kutoka TIPER, ikiwa ni gawio la hisa katika hafla iliyofanyika leo, mjini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER, Daniel Belair, wa pili kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER, Prof. Abdulkarim Mruma na wa kwanza kulia ni Kaimu Msajili wa Hazina kutoka Wizara ya Fedha, Elius Mwakabinga.


Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER, Daniel Belair (kushoto) akitoa taarifa ya kampuni ya TIPER invyoshirikiana na Serikali katika kukuza uchumi na kuongeza soko la ajira nchini, wakati wa kukabidhi gawio linalotolewa na kampuni yake kwa Serikali leo, mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER, Prof. Abdulkarim Mruma.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER, Daniel Belair (kushoto) akitoa taarifa ya kampuni ya TIPER invyoshirikiana na Serikali katika kukuza uchumi na kuongeza soko la ajira nchini, wakati wa kukabidhi gawio linalotolewa na kampuni yake kwa Serikali leo, mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER, Prof. Abdulkarim Mruma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Servarcius Likwelile (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER, Daniel Belair (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza katika hafla ya kupokea gawio la hisa za Serikali, mjini Dodoma leo. Wanafuata ni baadhi wa Maofisa Waandamizi wa Wizara Fedha. (Picha zote na habari na Ingiahed Mduma na Eleuteri Mangi-Wizara ya Fedha)
 
Na mwandishi wetu, Dodoma, 13/6/2014
SERIKALI imepokea shilingi bilioni moja kutoka TIPER ikiwa ni gawio ambalo kampuni hiyo imekuwa ikilipa kwa Wanahisa wake kila mwaka.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius Likwelile alipokuwa akipokea gawio hilo katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma.

Dkt. Likwelile alisema kuwa gawio hilo litaelekezwa kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha 2013/2014 unaomalizika kwa kuangalia maeneo ambayo yanawagusa wananchi ikiwemo sekta ya elimu, afya na maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Daniel Belair alisema kuwa si mara ya kwanza kwa kampuni yake kutoa gawio kama hilo kwa Serikali ambapo mwaka jana muda kama huu kampuni ilitoa kiasi kama hicho kama gawio

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kampuni yake imeendelea kufanya vizuri katika kukuza maisha ya kijamii na kiuchumi ambapo kwa sasa inafanyakazi kwa saa 24 na siku saba za wiki.

Kwa kuzingatia utendaji huo, kampuni ya TIPER imekuwa kichocheo kukuu cha kuzalisha ajira nchini ambapo hadi sasa asilimia 99 ya wafanyakazi wake ni nguvu kazi ya Watanzania.

Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma alisema kuwa imekuwa ni muhimu kwa kampuni yao kuwa na akiba ya kutosha ya mafuta kwa nchi na kuleta mafanikio makubwa ya upatikanaji wa mafuta nchini.

 Aidha, TIPER Prof. Mruma alisema kuwa kwa sasa kampuni yao imejikita katika kuleta mafuta yaliyosafishwa nchini ili kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

“Kwa sasa tunaleta mafuta yaliyosafishwa badala ya mafuta ghafi ambayo yanazalisha tope jingi ambalo limekuwa ni hatari katika kutunza mazingira yetu” alisema Prof. Mruma

Pamoja na ufanisi huo, kumekuwepo na changamoto za kuboresha mkataba wa utendaji na usimamizi wa hesabu masuala ambayo wanahisa wote wawili wanaendelea kuyafanyia kazi kwa madhumuni ya kuwa na matokeo mazuri zaidi kwa pande zote.

Kiutendaji kampuni ya TIPER inaendeshwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania ambayo inahisa zenye asilimia 50 na Kampuni ya Oryx Energies SA asilimia 50.
                                                                                                                
Pamoja na Tanzania Kampuni ya Oryx Energies SA inafanyakazi katika mnchi mbalimbali duniani ambazo ni Benin, Burkina Faso, Côte d'Ivoire, Guinea Conakry, Kenya, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Afrika Kusini, Uhispania (Visiwa vya Canary), Togo,  Uganda na Zambia.

No comments:

Post a Comment