*Kuzikwa kesho Kisutu jijini
Bondia Iraq Hudu wakati wa uhai wake
BONDIA wa zamani wa ngumi za kulipwa nchini, Iraq Hudu 'Kimbuga' (49) amefariki dunia leo, baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Dada wa Marehemu Tiba Takadiri, alisema kuwa Hudu amefariki usiku wa kuamkia leo, majira ya saa 11 ya alfajiri kwenye hospitali ya Hindu Mandal, alikokuwa amelazwa.
Takadiri, alisema kuwa mazishi ya Hudu yatafanyika kesho kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ini na figo kutofanya kazi, ambapo vilimsumbua kwa muda mchache kabla ya kufariki kwake.
"Marehemu alilazwa hospitali Hindu Mandal siku tatu zilizopita, ambapo majuzi jioni alizidiwa na leo asubuhi kukutwa na umauti.
Hudu amezaliwa mwaka 1965, Ujiji Kigoma na kupata elimu ya msingi mkoani humo na baadaye kuja jijini Dar es Salaam ambapo alimaliza Shule ya Sekondari na baadaye kuanza shughuli za ngumi katika miaka ya 1990 mpaka miaka ya 2000 alipoacha.
Marehemu ameacha watoto watatu, ambao ni Daniel alikuwa akitarajia kufunga ndoa Juni 20, wakati mtoto mwingine Msawila ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita.
Maandalizi ya msiba yanaendelea nyumbani kwa marehemu Buguruni Rozana Dar es Salaam ambapo kesho saa 7, atazikwa Kisutu.
Marehemu Hudu aliwahi kutamba akiwa na mabondia akina Joseph Marwa, Stanley Mabesi, na baadaye wakaja mambondi wengine, akiwemo Rashid Matumla na Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo'.
No comments:
Post a Comment