TANGAZO


Thursday, June 26, 2014

Red's Miss Changombe 2014 zawadi zatajwa

Mratibu wa Shindano la kumtafuta mrembo wa Redd’s Miss Chang’ombe, Tom Chilala (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa kuitangaza zawadi za washindi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco na Ofisa Uhusiano  wa TV1, Mponjoli Katule. 
Warembo wa shindano la Redd’s Miss Chang’ombe wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa shindano hilo, wasanii watakaotoa burudani siku ya fainali. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo.
 Ofisa Uhusiano  wa TV1, Mponjoli Katule (wa tatu kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wa TV1 katika shindano la Redd’s Miss Chang’ombe.
Rapa wa bendi ya Ruvu Stars, Msafiri Diouf ‘Sokoine’ akighani wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Warembo wakiwa wamepozi kwa picha.
 
Na Mwandidhi Wetu
MNYANGE atakayevishwa taji la Redds Miss Temeke  2014 linalotarajia 
kufanyika Juni 27 mwaka huu katika  ukumbi wa TTC Chang’ombe anatarajia 
kujinyakuria  kitita cha sh. laki tano. 
Mshindi wa pili atajinyakulia laki 
tatu, mshindi wa tatu  laki mbili na washiriki wengine watapata kifuta 
jasho cha sh. 65,000.

Mratibu wa shindano hilo 
Tom Chilala, alisema katika  shindano hilo anatarajia kumtoa mrembo  
atakafanikiwa  kutwaa taji la misi Tanzania mwaka huu hapo baadaye.

“Mwaka huu nina warembo wazuri na wenye vigezo vyote, naamini mwaka 
huu nitarudisha heshima yangu ya  kufanikiwa
kutoa warembo kutoka Redd’s Miss Temeke hadi Redd’s Miss Tanzania,” alisema.
 
 Alisema
mwaka 2010 alifanikiwa kumtoa Genevieve Emmanuel, kutoka miss Temeke hadi 
miss Tanzania,  hivyo na kwa mwaka huu anaamini itakuwa hivyo kutokana na warembo alionao. 
 

Aidha shindano hilo litakarokuwa na washereheshaji kutoka bendi ya Ruvu 
Stars, Mchekeshaji Kitale pamoja na msanii anayetamba na kibao cha Basi Nenda Moshi Katena na wengine. Kiingilio katika shindano hilo kitakuwa ni sh. 20,000 kwa VIP na Elfu 10000 kawaida. 
 
Naye Mkurugenzi wa 
Marie Stoper John Bosco ambao ni wadhamini wa shindano hilo alisema
wameamua kudhamini mashindano hayo kwa lengo la kuwaelimisha vijana
kuhusiana na uzazi wa mpango. 
 
Alisema hawataishia hapo wanaendelea kudhamini hadi
miss Tanzania kutokana na kuona vijana hao wanaweza kuliwakilisha taifa.”Katika 
sensa viijana ndio wameonekana kuwa na asilimia kubwa hivyo ni vizuri kuwa 
dhamini ili kuweza kujenga kizazi ambacho kimewezeshwa ambacho hakitaweza
kuwa taifa tegemezi,” alisema.

No comments:

Post a Comment