Kamimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee akizungumza na
wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwenye hoteli ya Oceanic Bay
mjini Bagamoyo asubuhi hii wakati wa seina inayojadili masuala
mbalimbali yakiwemo mafanikio ya mfuko huo, malengo na Changamoto zake
katika kufanikisha huduma ya afya kwa jamii, ambapo uwigo wa walengwa
katika huduma hizo umeongezeka kutoka kaya 120 mwaka 2009 na kufikia
kaya 668.474 mwaka 2014 sawa na wanufaika milioni 4.01 na mpaka sasa
mfuko huo unafanya kazi na Halmashauri za wilaya 129 katika nchi nzima
kati ya Halmashauri 168 zilizopo lakini pia tayari Halmashauri 20 kati
ya hizo zimeshahamasishwa na zitaingia katika mpango huo siyo muda
mrefu. (Picha zote kwa hisani ya Kikosikazi cha Fullshangwe-Bagamoyo)
Eugen
Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji akitoa mada katika semina hiyo juu ya
uchangiaji wa huduma za mfuko wa bima ya afya kulia ni Raphael Mwamoto
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti na katikati ni Rehani Athman Kaimu Mkurugenzi wa mfuko wa afya ya Jamii (CHF)
Dk Frank Lekey Mkurugenzi wa Huduma za
Tiba na Kitaaluma akitoa mada kuhusu uboreshaji wa huduma za mfuko wa
Afya ya jamii ambapo kwa sasa wanafanya kazi na hospitali za serikali na
baadhi ya hospitali za mashirika ya dini.
Rehani Athman
Kaimu Mkurugenzi wa mfuko wa afya ya Jamii (CHF) akizungumzia
mafanikio yaliyokwishapatikana kutokana na huduma za mfuko wa Afya ya
jamii.
John Bwire Mkurugenzi wa kampuni ya Raia
Mwema na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia mada
mbalimbalzinazotolewa katika semina hiyo.
Mhariri Dany Mwaijega na wenzake wakifuatilia majadiliano ya semina hiyo.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari Bw. Absalom
Kibanda akizungumza katika semina hiyo inayofanyika mjini Bagamoyo
anayefuata ni Abdalla Majura kutoka ABM Radio.
Mhariri wa Gazeti la Mawio Jabir Idrissa akitoa mchango wake wakati wa majadiliano katika semina hiyo.
Kamimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee na viongozi
wengine wa mfuko huo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kufunguliwa rasmi mjini Bagamoyo.
Wahariri mbalimbali wakibadilishana mawazo mara baada ya kufungua semina hiyo.
Kulia ni Anna Mhina Katibu Mhutasi na Hawa Diguza Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wakiwa katika picha ya pamoja.
Kulia
ni Anna Mhina Katibu Mhutasi katikati ni Hawa Diguza Afisa Masoko na
Elimu kwa Umma na Anna Mziray Meneja wa Msoko na elimu kwa umma wakiwa
katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment