Mwanamuziki
Mkongwe wa Rege nchini, Innocent Nganyagwa akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusiana na show yake kwenye tamasha la ZIFF
2014 usiku wa leo ndani ya ukumbi wa Mambo Club kwenye viunga vya Ngome
Kongwe visiwani Zanzibar.Kushoto Mtaalamu wa masuala ya habari ZIFF, Bw. Dave Ojay. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Baadhi
ya wageni mbalimbali na waandishi wa habari wanaohuduria tamasha la
ZIFF 2014 linaloendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar.
BAADA
ya kutoa demo katika mkutano wake na waandishi wa habari, mkali wa rege
nchini Innocent Nganyagwa ameahidi kuporomosha muziki mzito katika
ukumbi wa mambo klabu leo usiku.
Katika
demo ambapo alipiga verse ya gila, mkali huyo aliwataka wazanzibari
kuingia kwa wingi kuona sweet reggae baada ya mfumo wa Babylion wa
ukombozi kumalizika.
Anasema
kwamba wapenzi wake watarajie vitu vipya kuonesha kwamba yeye hajalala
kwa miaka yote hata baada ya kuonekana kuwa nje kwa miaka 9.Nganygwa
mwenye tuzo tano za nyumbani na albamu nne katika mikono amesema
kwamba kimya chake kilitokana nba kuamua kusuka kizazi kipya cha rege
kupitia kampuni yake ya Reggae Production.
Akizungumza
kuhusu muziki wake alisema kwamba yeye anapiga muziki wa rege lakini si
kwa mtazamo wa Jimmy Clief,Bob marley na Burning Spear ; ni muziki
wenye utamaduni wa nyumbani na hivyo kwua na rege yenye utambulisho wa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment