TANGAZO


Thursday, June 19, 2014

Bimu lililookotwa na watoto Mtwara



Hili ni ndilo bomu ambalo jioni ya June 16 2014 kwenye kijiji cha Mdui, Kata ya Mawala, Wilaya ya Mtwara Vijijini Mkoa wa Mtwara, liliokotwa na watoto waliokua wakicheza karibu na eneo la Makaburi.
Askari wa JWTZ, akiliangalia bomu ambalo liliokotwa na watoto waliokuwa wakicheza karibu na eneo la Makaburi, jioni ya June 16 2014 katika Kijiji cha Mdui, Kata ya Mawala, wilayani Mtwara Vijijini, Mkoa wa Mtwara. Taarifa iliyotolewa na Polisi baadaye, ambapo baada ya wataalamu kuja na kuchunguza waligundua ni bomu la kurusha kwa mkono ambalo lina namba TNT MORTAR BOMB 60MM,LOT SOL 618, ambapo Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi walichukua hatua za kiusalama na kwenda kulilipua porini.  

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga ameongea na kusema, "ukiliangalia ni bomu ambalo ni la muda mrefu, nadhani ni kipindi kile cha vita vya Msumbiji. Tulilipeleka porini likalipuliwa na ulipuaji wake haukuwa na madhara… na sio kwamba ni bomu tunaweza kusema limeletwa ama imekuaje, ni bomu la muda mrefu tu", alisema.
Askari wa JWTZ, akiwa amelishikilia bomu hilo, huku akitoa tabasamu. Bomu hili ambalo liliokotwa na watoto waliokuwa wakicheza karibu na eneo la Makaburi, jioni ya June 16 2014 katika Kijiji cha Mdui, Kata ya Mawala, wilayani Mtwara Vijijini, Mkoa wa Mtwara, ambapo baada ya wataalamu kuja na kuchunguza waligundua ni bomu la kurusha kwa mkono ambalo lina namba TNT MORTAR BOMB 60MM,LOT SOL 618, ambapo Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi walichukua hatua za kiusalama na kwenda kulilipua porini.
Baadhi ya Maaofisa kutoka jeshi la Wananchi wa Tanzania wakilitazama bomu hilo.

No comments:

Post a Comment