Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Mohamed Ghalib Bilal kulia akifuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa
wakati wa Uzinduzi wa Kongamano la Confucius Barani Afrika jana jijini Dar es
Salaam, kushoto ni Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Watu wa China Li Yuanchao.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mlimani ya jijini Dar
es Salaam wakitoa burudani katika uzinnduzi huo kwa kuimba nyimbokwa lugha ya
kichina.
Baadhi ya wageni wakifuatilia kwa makini burudani
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa Uzinduzi wa Kongamano la Confucius
Barani Afrika jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China Li Yuanchao akioneshwa machapisho mbalimbali yanayohusu Utamaduni wa watu
wa China.
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China Li Yuanchao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed
Ghalib Bilal wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa wakati
wa Uzinduzi wa Kongamano la Confucius Barani Afrika jana jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li
Yuanchao akisalimiana na Mke wa Baba wa Taifa mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea
nyumbani kwake jana ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akimkabidhi zawadi Mama Maria Nyerere jana wakati alipomtembelea nyumbani kwake Msasani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafamilia ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Ghalib Bilal kushoto na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao wakimwaga mchanga kwenye jiwe la msingi mahali ambapo ubalozi wa China unatarajiwa kujengwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Ghalib Bilal na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakandarasi wa mradi huo wa ujenzi wa Ubalozi wa China nchini Tanzania.
Burudani zikiendelea wakati wa kuweka jiwe la msingi
mahali ambapo ubalozi wa China unatarajiwa kujengwa mapema jana jijini Dar es
Salaam. (Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO)
No comments:
Post a Comment