Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasirimali Tanzania, Joseph Rweyemamu (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari, leo jijini Dar e s Salaam kuhusu maonesho ya 15 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo kama Nguvu kazi/Jua Kali yanayotarajiwa kuanza 30 hadi Desemba 7 mwaka huu. Kushoto ni Afisa Kazi Mwandamizi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Sara Daudi.
Mratibu wa Chama cha Utabibu wa Dawa Asili Tanzania, Boniverntura Ferdinand (katika), akiwaeleza umuhimu wa dawa asilia wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu maonesho ya 15 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo kama Nguvu kazi/Jua Kali yanayotarajiwa kuanza Novemba 30 hadi Desemba 7 mwaka huu, kulia ni Afisa Habari Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema na kushoto ni Mweka Hazina wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Tanzania, Jumbe Ngutto. (Picha zote na LoriethaLaurence-Maelezo)
Lorietha Laurence-
Maelezo
17/06/2014
WAJASIRIAMALI wamehimizwa kujiandikisha kwa wingi ili waweze kushiriki katika maonesho ya 15
ya wajasiriamali ya sekta isiyo rasmi yanayoshirikisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo kama
Nguvu ya kazi/Jua kali yanayotarajiwa kufanyika November 30 hadi desemba 7,
2014 mjini Kigali Rwanda.
Wito huo umetolewa na
Afisa Habari Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira,
Ridhiwani Wema alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar
es salaam na kusema kwamba lengo la kuwahimiza wajasirimali kuweza kujitangaza
nje ya nchi na kupanua wigo wa soko la bidhaa zao linadhamiria kuongeza ajira.
“naowaomba
wajasiriamali waweze kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha na hivyo kuweza
kushiriki maonesho haya ambayo yatajumuisha nchi za Afrika Mashariki na hivyo
kuwapa fursa ya kupanua wigo wa soko kwa bidhaa zinaotengenezwa na wajasiriamali
hao,” alisema Ridhiwani.
Aliongeza kuwa maonesho hayo yana malengo ya kuongeza fursa
za ajira kupitia uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, kuchochea ubunifu, kupanua
wigo wa masoko na kuwaunganisha wajasiriamali wadogo katika ngazi ya nchi na
Afrika Mashariki kwa ujumla.
Aidha alisisitiza kuwa ili mjasiriamali aweze kushiriki katika
maonesho hayo ni lazima awe mzalishaji wa bidhaa inayohitajika katika maonesho,
pia bidhaa hizo ziwe zenye ubora kwa
kukubalika na ubora wa viwango (TBS) na viwango
vya taasisi inayosimamia vyakula dawa,TFDA, kadhalika anuani ya kudumu ya
mahali anapofanyia kazi mjasiriamali husika.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya
Wajasiriamali Tanzania, Joseph Rweyemamu aliongeza kuwa kuna umuhimu sana kwa
wajasiriamali kushiriki maonesho haya kwa sababu ni njia mojawapo ya
kujitangaza nje ya nchi kutokana na bidhaa
zao.
Maonesho hayo yalianzishwa
mwaka 1999 jijini Arusha, wakati wa
kusainiwa kwa mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na yamekuwa yakiendelea kufanyika kila mwaka
kwa kuzunguka nchi zote za Afrika Mashariki, ambapo kwa Tanzania bara
yalifanyika mwaka 1999,2006 na 2009.
No comments:
Post a Comment