Meneja Mauzo wa kampuniya Bima ya Jubilee Tanzania, Bw. David Ludovick (kushoto), akitoa maelezo ya kina kwa mmoja wa wananchi waliojitokeza katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari katika kilele cha siku ya uchangiaji damu duniani, zoezi hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mlimani City jijini.
Mmoja wa wauguzi kutoka Mpango wa Taifa wa damu salama akimpima mmoja wa wakaazi wa jijini aliyejitokeza katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, zoezi hilo lilifanywa kwa ushirikiano wa Mpango wa Taifa wa Damu salama na Kampuni ya Bima ya Jubilee Tanzania.
Ofisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Bi. Selina Sahani akimtoa damu Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Tanzania Bw. David Ludovick katika viwanja vya Mlimani City mwishoni mwa wiki, zoezi hilo la uchangiajia damu kwa hiari lenye kauli mbiu “Damu salama kwa ukombozi wa akina mama” liliadhimishwa kwa ushirikiano chini ya Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama na Kampuni ya Bima ya Jubilee Tanzania.
Baadhi ya wahudumu kutoka Mpango wa Taifa wa damu salama wakitoa maelekezo na upimaji wa wingi wa damu kwa wakaazi wa jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu kwa hiari duniani, zoezi hilo lenye kauli mbiu “Damu salama kwa ukombozi wa akina mama”limefanywa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Tanzania na Mpango wa Taifa wa damu salama nchini.
Baadhi ya wahudumu kutoka Mpango wa Taifa wa damu salama wakitoa maelekezo na upimaji wa wingi wa damu kwa wakaazi wa jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu kwa hiari duniani, zoezi hilo lenye kauli mbiu “Damu salama kwa ukombozi wa akina mama”limefanywa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Tanzania na Mpango wa Taifa wa damu salama nchini.
KILA mwaka tarehe 14 Juni ni siku ya kuchangia damu
duniani, Jubilee Insurance chini ya idarayakeya utabibuikishirikiana na wizara
yaafyaTanzania na ustawi wa jamii (National Blood Transfusion) Ningependa kuchukua fursa hii kuwakaribisha Watanzania wote katika
kuokoa maisha kwa kuchangia damu katika hafla itakayofanyika Mlimani City tarehe
14 Juni 2014 kuanziasaa 2 asubuhi mpaka saa 8 mchana.
Mbiu ya mwaka
huu ni "Damu salama kwa ukombozi wa akina mama."
1. Kwa nini ni Jubilee
Insurance inafanya hivi? -
Jubilee Insurance ikiwa sehemu ya jumuiya ya
kimataifa, inawajibu wa kuchangia katika sekta ya afya na maisha ya wanajamii.
Tunathamini sana maisha ya kaka na dada zetu, ila zaidi ni mateso na
maumivu wapatayo akina Mama katika kutuhudumia sisi.
2. Jubilee Insurance imehusika
katika shughuli hii kwa muda gani?
Hii ni mara ya pili kwa hapaTanzania, mara ya kwanza walichangia wafanyakazi wetu,
ambapo TNBS walikuja ofisi za Jubilee kwa ajili ya mchango wa damu,
wafanyakazi wengi walishiriki
3. Shughuli gani nyingine Jubilee
Insurance imewahi kufanya kabla ya hii?
Kama Kampuni ya bima, Jubilee Insurance hutoa huduma zote zitolewazo na
bima, miongoni mwa huduma hizo ni bima za matibabu, bima za magari na zisizo za
magari, bima za moto na kadhalika.
4. Jubilee
wana lengo gani kutokana na Hafla hii ?
Lengo ni kuleta watu wenye nia njema pamoja, waweze kuchangia
damu zao kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama - tunaelewa hatari kubwa inayowakabili
akina mama kabla na baada ya kujifungua. Kina mama hupoteza damu nyingi. Matokeo yake ni kupoteza
maisha. Jubilee inajitahidi kutokomeza suala hili.
No comments:
Post a Comment