TANGAZO


Thursday, June 26, 2014

Gazeti la Citizen latakiwa kuomba Radhi


Professa Hassan Bical Mshauri katika Bodi ya Chuo akionesha baadhi ya Nakala ya Gazeti la Citezens lilivyoandika habari zisizo za ukweli, kushoto ni Nabeel Almandhy

WAANDISHI wa habari na Mhariri wa gazeti la Citizens wanakurupuka kuandika stori bila ya kufanya uchunguzi wa kina juu ya habari wanazopata, pamoja na kuhoji upande wa pili wa wahusika.

Hayo yalisemwa na Professa Hassan Bical Mshauri wa Bodi ya chuo cha Cyprus baada ya gazeti hilo kuandika makala ya chuo hicho hakitambuliki hapa nchini na nje ya nchi na wanafunzi 200 wanasoma chuo hicho taaluma inayotolewa katika chuo hicho na vyeti ni feki, kwa kufuatia kuandika kwa taarifa hiyo, gazeti la Citizen wamepewa saa 48 kuanzi sasa kuomba radhi kwa kuandika kitu ambacho cha uwongo.

Kama hawajaomba radhi kwa saa hizo basi gazeti hilo watalipeleka Mahakamanikwa kuandika habari za uwongo, ambazo hazijafanyiwa uchunguzi.

"Wanatakiwa kuandika makala za uchunguzi sio kukurupuka na kuandika stori bila ya kuwa na uhakika wa ukweli wa stori hiyo, na wasichanganye mambo ya elimu na siasa wanatakiwa wajue kuwa elimu ni kitu cha msingi sana kwa nchi ya Tanzania na siasa ni siasa tu."Alisema Professa Bical.

 Aidha kabla ya kuitisha mkutano Professa alipiga simu kwa mara ya kwanza ilipokelewa lakini hawakuelewa na aliyepokea simu, alipiga simu mara ya pili lakini simu haikupokelewa, ndio akaamua kuitisha mkutano huo.

Chuo hicho kwa sasa kinatambulika na umoja wa vyuo vikuu duniani (INQAAHE) lakini pia kuna wanafunzi 70 kutoka nchi mbalimbali duniania, chuo cha 641 kujulikana duniani pamoja na kinawakilisha nchi 120 duniani.

No comments:

Post a Comment