WAZIRI wa Habari Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara amewatumia salamu za rambirambi waandishi wa habari kufuatia kifo cha Mpiga picha wa kituo cha television cha Mlimani, Ndugu Maximilian John kilichotokea alfajiri ya kuamkia Jumamosi wiki iliyopita.
Dkt.
Mukangara amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Bwana
Maximilian kilichotokana na maradhi ya Moyo, Sukari na Shinikizo la damu na ameongeza kuwa kifo
hicho ni pigo na pengo kubwa kwa tasnia ya habari hapa nchini.
Amesema Bw.
Maximilian atakumbukwa kwa uchapakazi na uhodori wake wa kazi zake uliokuwa
unazingatia weledi wa taaluma ya uandishi wa habari, jambo lililomfanya awe na
marafiki wengi wa tasnia hiyo.
“Nakutumia
salamu zangu za dhati kuomboleza msiba huu mkubwa kwa watumishi wote wa Mlimani
TV, tasnia ya habari na familia yake kwa ujumla, amesema Dkt. Mukangara.
Ameongeza
kuwa Bw. Maximilia atakumbukwa daima na waandishi wa habari na wadau wengine
kwa ucheshi wake,ushirikiano na wenzake wakati wa kutekeleza majukumu ya
kitaalum na ujenzi wa Taifa kupitia Sekta ya habari.
“Ninaungana na waandishi wa habari na wadau
wengine katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya
marehemu. Amen,” amesema Dkt.Mukangara.
Imetolewa
na;
IDARA YA HABARI, VIJANA , UTAMADUNI
NA MICHEZO
26 Mei, 2014
No comments:
Post a Comment